Home Kitaifa JICHO LA 3: KWA USAJILI HUU, OMOG AMESHAFUKUZWA SIMBA SC, BADO…

JICHO LA 3: KWA USAJILI HUU, OMOG AMESHAFUKUZWA SIMBA SC, BADO…

1984
0
SHARE

img_0077.jpg

Na Baraka Mbolembole

Ni ‘upuuzi’ mtupu. Wala hakuna jipya kwa wachezaji watakaounda kikosi cha Simba SC msimu wa 2016/17. Kigezo cha kwanza kitakachoendelea mwenendo mbaya wa timu ni usajili ambao tayari umefanywa na ‘Mr.Kazinyingi’ na kocha mpya atapaswa kufanya kazi na wachezaji hao huku akipata matokeo, vinginevyo atafukuzwa ‘bila huruma.’

Mimi si kocha, lakini sikubaliani na usajili wa mlinzi wa kati raia wa DR Congo, Janvier Besala Bokungu . Huyu ni mchezaji aliyeichezea timu yake ya Taifa mara 9 katika kipindi cha miaka 9 sasa. Katika nafasi ya Mcongo huyu ni heri kabisa wangeendelea kubaki na Hassan Isahaka ‘aliyeondolewa kwa chuki binafsi.’

Emmanuel Simwanza si mchezaji wa ligi kuu msimu wa 2016/17 na Novatus Lufunga bado si mchezaji wa kuipa Simba mataji hivi sasa, labda kwa hapo baadaye kama ataendelea kutunzwa vizuri huku yeye mwenyewe akipandisha zaidi kiwango chake cha uchezaji.

Kuna baadhi ya wana-Simba wamekuwa wakilinganisha kikosi chao kipya na kile cha mahasimu wao Yanga SC! Wanashangaza sana, labda yatokee maajabu kama yale yaliyofanywa na Leice ster City pale England-kushinda taji wakiwa na kikosi chenye thamani ndogo.

Usiwalinganishe kabisa kikosi cha thamani ya juu kama cha Yanga na kikosi cha ‘bure’ kilichosajiliwa na ‘Mafionso-Genge la Wahuni.’ Yanga wapo katika daraja lingine kabisa, kimpira, kiutawala na kimafanikio. Kwa miaka miwili mfululizo sasa wamekuwa wakicheza kitimu zaidi licha ya kuongeza baadhi ya wachezaji wapya na kuwaacha wengine katika nafasi muhimu wanapoona mapungufu.

Jambo hili halipo kabisa ndani ya timu ya Simba. Unaweza kugundua hilo hata bila kutafakari, kwa maana mchezaji aliyeinyanyua zaidi timu hiyo kiufungaji msimu uliopita, Mganda, Hamis Kizza ametemwa, eti anakuja mchezaji aliyejipa thamani ya milioni 100 mwaka mmoja uliopita.

Ila sasa anakuja bure. Kuna mengi sana yamebadilika katika klabu ya Yanga. Kwa mara ya kwanza nilianza kulitumia jina la ‘Mr.Kazinyingi’ katika makala zangu, nikiwalenga wale ‘jamaa ambao hawakuwa na ufahamu ‘ na mambo ya mpira walipowasaini Mganda, Emmanuel Okwi na Hassan Dilunga katika timu ya Yanga mwezi Disemba, 2013.

Usajili ule ndiyo ulimuondoa mkufunzi, Ernie Brandts baada ya kuwaambia waajiri wake ‘Sikuwahitaji na Okwi na Dilunga.’Yanga sasa hakuna ‘Mtu aliye na ujuzi na mamlaka ya kufanya chochote, tena akijipa majukumu hayo yeye mwenyewe.’

Lakini ndani ya Simba mtu huyu yupo, tena ana nguvu, pesa na mamlamka makubwa kuliko rais wa klabu. Sasa amepata msaidizi makini, ambaye yeye huwa ni mtu wa kukurupuka na hasira zaidi. Kumuacha Kiiza na kumsaini Mavugo ni kamari nyingi ya kupoteza ambayo Zacharia Hans Poppe ameicheza tena akiwa kinara wa kamati ya usajili.

Ukiangalia majina ya mchezaji mmojammoja na nafasi zao wanazocheza, Simba itandelea kuburuzwa na Yanga na si ajabu ushindani mkubwa zaidi kwa timu hiyo ya Msimbazi utakuwa miongoni mwa timu tano bora.

Kwenye uchambuzi wa kwenye makaratasi unaweza kuona kikosi kinatisha kwa sababu yapo majina kama ya Ame Ally, Mavugo amnayempenda, Salum Kimenya, Shiza Kichuya, Mbaraka Yusuf, Hamadi Juma, Muzamir Yassin, Hassan Kabunda , Mohamed Ibrahim, lakini ndani ya uwanja kocha Joseph Omog hatasaidiwa.

Sababu nyingine itakayoipoteza Simba msimu ujao ni kocha mwenyewe, Omog. Unaweza kusema ni kocha mzuri kulingana na rekodi zake ila kimbinu, na kwa namna ya Simba ichezavyo Mcameroon huyu ataanguka tu ndiyo maana kwa mara ya kwanza rais wa klabu Evance Aveva amekiri katika utambulisho wa kocha mpya mbele ya wana-habari kuwa ‘watamfukuza’ ikiwa timu itashindwa kupata matokeo.

Omog amepelekwa Simba na katibu mkuu mpya ambaye ni marafiki na ndiye aliyependekeza Mcameroon huyo apewe Azam FC miaka miwili iliyopita. Simba hawakuwa na mpango na Omog ila ameletwa na rafiki yake na sasa ‘kategewa bomu la masaa.’

Simba wamesaini timu ya kushindana na Mbeya City FC, Tanzania Prisons, Mwadui FC, Mtibwa Sugar na si Yanga na Azam FC. Omog kwanza atalazimika kutafuta uwiano ulio sawa kati ya wachezaji wapya wengi, na wachache waliobakizwa ili ajue ni aina gani ya soka wanalopaswa kucheza.

Hadi afanikiwe katika hilo, walio bora hivi sasa watakuwa mbele yao tu. Na si wengine ni Yanga na Azam. Kwa usajili huu, Omog ameshafukuzwa Simba SC, bado kupewa barua yake tu….

Kwa ukaribu zaidi, tafadhali unaweza ku-LIKE PAGE yangu BSports. Utapata Updates za michuano mbalimbali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here