Home Dauda TV Video: MESSI AMEAMUA KUSTAAFU TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA

Video: MESSI AMEAMUA KUSTAAFU TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA

591
0
SHARE

Messi-Kustaafu

Chile wameshinda taji la Copa America kwenye mchezo wa alfajiri ya ya kuamkia Jumatatu June 27 baada ya kuifunga Argentina kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Messi alikosa penati kwenye hatua ya matuta, ni mara ya pili ndani ya miaka miwili mfululizo Argentna kupoteza mchezo wa fainali ya Copa America mbele ya Chile ‘La Roja’.

Argentina imepoteza mchezo wa fainali kwa mara ya tano sasa mfululizo. Kombe lao la mwisho kwenye michuano mikubwa lilikuwa ni Copa America mwaka 1993.

Kufuatia kipigo hicho dhidi ya Chile, Leo Messi ameamua kuachana na timu yake ya taifa ‘amestaafu kukitumikia kikosi cha Albiceleste.

Baada ya game dhidi ya Chile, nyota huyo mwenye miaka 29 amekiambia kituo cha TYC Sports kwamba, amaisha yake ya soka la kimataifa yamefika mwisho.

Kwasasa timu ya taifa basi tena. Baada ya kupoteza fainali nne sitaendelea tena kuitumikia timu ya taifa. Naamini tayari maamuzi yameshafanyika. Nimechukua muamuzi huu kwa ajili yangu pamoja na watu wengu waliotaka iwe hivi. Nimepambana sana, lakini ninaondoka nikiwa sijafanikiwa.

Messi atabadili maamuzi yake? Au ndiyo basi tena na amemaliza maisha yake ya soka bila kushinda kombe la dunia?

Video-Messi akitangaza uamuzi wa kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Argentina

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here