Home Kitaifa Huu ndio usajili mpya wa Simba SC katika safu ya uongozi.

Huu ndio usajili mpya wa Simba SC katika safu ya uongozi.

3272
0
SHARE

Wakati timu mbalimbali zinazoshiriki katika ligi kuu ya Tanzania vikiwa vinajiandaa na kujiimarisha katika usajili wa wachezaji mbalimbali kwenye vikosi vyao – klabu ya Simba imeripotiwa kufanya usajili mwingine, lakini safari hii usajili wao ni kwenye safu ya uongozi wa timu yao.

 Taarifa za ndani kutoka katika klabu ya Simba zinasema kwamba, Rais wa klabu hiyo Evans Aveva amemteua aliyekuwa mratibu na meneja wa klabu ya Azam FC, Bwana Patrick Kahemele kuwa katibu mkuu wa Simba.

 Mtandao huu ulimtafuta Patrick Kahemele kuzungumzia juu ya uteuzi wake wa kushikilia nyadhifa hiyo ndani ya klabu ya Simba: “Sina hiyo taarifa mpaka sasa, sifahamu lolote na ndio maana siwezi kuzungumzia jambo hilo,” alisema Kahemele.

Taarifa ambazo mtandao imezipata zinasema Uteuzi wa Kahemele unatarajiwa kutangazwa hivi karibuni na Aveva baada ya taratibu zote kukamilika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here