Home Kimataifa BBC WAWASAJILIA ARSENAL VARDY

BBC WAWASAJILIA ARSENAL VARDY

538
0
SHARE

 

Vardy-England 4

Moja ya mitandao mikubwa ya habari ulimwenguni wa BBC jana ulishtusha ulimwengu baada ya Jamie Vardy kuifungia England goli la kusawazisha kabla ya Daniel Sturridge kuongeza la pili na kuipa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wales ya kina Bale.

Je, waliteleza kwa kile walichokifanya jana?

Stori iko hivi…baada ya Vardy kufunga goli hilo la kusawazisha, BBC walimripoti Vardy kama mchezaji wa Arsenal.

Haijaeleweka bado kama kweli Vardy amekamilisha usaijili wa kujiunga na Arsenal kimyakimya au BBC waliteleza tu kwa bahati mbaya.

Ikumbukwe tu, kabla ya Vardy kusafiri na England kwenda Ufaransa kwa ajili ya michuano ya Euro, Arsenal walionesha nia ya kumsajili Vardy na hata kukidhi mahitaji ya ada ya usajili, lakini mshambuliaji huyo wa Leicester hakuwa tayari kufanya maamuzi hadi michunao ya Euro itakapomalizika.

Huu ndiyo ushahidi wenyewe kutoka BBC

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here