Home Kitaifa #EURO 2016: LEO NI VITA YA NDUGU WAWILI, AUSTRIA VS HUNGARY

#EURO 2016: LEO NI VITA YA NDUGU WAWILI, AUSTRIA VS HUNGARY

428
0
SHARE

Autria vs Hangury

Leo michuano ya Euro inaendelea tena nchini Ufaransa, ambapo katika kundi F kutakuwa na kibarua kizito kati ya Austria na Hungary. Mchezo huu ambao utapigwa majira ya saa moja usiku kwa saa za Afrika Mshariki kunako dimba la Matmut Atlantique jijini Bordeaux, unabeba hisia kubwa sana kutokana na uhasimu wa pande hizi mbili.

Kipa wa Hungary Gabor Kiraly anatarajia kuweka historia mpya katika michuano hii. Akiwa na miaka 40 na siku 75, mkongwe huyo atakuwa kipa wa kwanza mwenye umri mkubwa kuweza kushiriki michuano hii, akimzidi kiungo wa zamani wa Ujerumani Lothar Matthaus, ambaye alicheza akiwa na umri wa miaka 39 na siku 91.

Kiraly amecheza mara 12 katika michezo ya awali ya kufuzu kuelekea michuano hii, ikiwa ni pamoja na ile ya hatua ya mtoano dhidi ya Norway ambapo vijana hao wa Bernd Storck waliweza kushinda kwa wastani wa mabao 3-1. Hata hivyo kocha wake anasema hana tatizo juu ya umri wa mchezaji huyo.

“Mara nyingi nimekuwa nikimwambia umri si suala muhimu kwangu,” Storck alisema. “Mimi huwa sijali kama mchezaji ana umri mkubwa ama kijana, muhimu ni yeye kufanya kazi yake kwa uhakika. Ni kipa mzuri, anajiamini na ana kipaji cha kukubalika kwa watu. Atatoa mchango mkubwa kwenye mafanikio ya timu katika michuano hii”.

Kwa mara ya mwisho, Austria ilishiriki michuano hii mwaka 2008, ambapo walishiriki kama nchi waandaaji, lakini mwaka huu wamekuja kwa kishindo bila ya kupitia mlango wa nyuma, baada ya kucheza michezo yao yote katika hatua ya awali ya kufuzu bila ya kufungwa.

Walishinda michezo tisa na kutoka sare mmoja katika michezo yao yote, wakizidiwa na England ambao walishinda michezo yote 10, na wamepachikiwa jina la farasi weusi na mchambuzi wa Sky Sports Matt Le Tissier.

Lakini licha ya yote hayo, wanatambua ugumu wa mchezo wa leo kutoka kwa wapinzani wao. Hivyo basi kiungo wao Alessandro Schopf anahitaji nguvu ya ziada kudhibiti eneo la kiungo na kusukuma mashambulizi ya nguvu ili kuipa matokeo timu yake.

“Kuhalisia utakuwa ni mchezo mgumu sana kwetu”, Schopf ambaye anakipiga kunako klabu ya Schalke amesema.

“Ni wapinzani wagumu, wana safu nzuri ya ulinzi . Safu yao pia iko vizuri kwasababu huwa wantengeneza nafasi nyingi sana. Tunapaswa kujitolea kwa asilimia 120 ama vinginevyo tukubali kutoshinda”.

Mchezaji wa Leicester City Christian Fuchs ndiye atakayeongoza jahazi la Austria, huku nyota wa Bayern Munich David Alaba akiwa fiti kabisa kutekeleza majukumu yake bila kusahau uwepo wa nyota wa Stoke City Marko Arnautovic.

Hofu kubwa iliyopo kwa kocha wa Austria Marcel Koller ni juu ya straika wake Marc Janko ambaye ndiye mfungaji wao bora katika hatua ya kufuzu akiwa na magoli, lakini taarifa za awali zinaeleza kuwa nyota huyo atakuwa fiti katika mchezo wa leo.

Kwa upande wa Hungary, kocha wao Bernd Storck atakuwa na wasiwasi juu ya uwepo wa nyota wake Krisztian Nemeth kutokana na kusumbuliwa maumivu ya misuli.

Dondoo muhimu

  • Hungary hawajafungwa katika michezo yao 3 ya mwisho dhidi ya Austria (wameshinda mara 2, sare moja).
  • Pambano lao kubwa lilikuwa ni mwaka 1934 katika fainali za Kombe la Dunia. Katika mchezo huo wa robo fainali, Austria walishinda 2-1.
  • Austria hawajafuzu kucheza michuano mikubwa duniani tangu mwaka 1998 (ukiondoa Euro ya mwaka 2008 ambayo wapata tiketi ya kushiriki moja kwa moja kama wenyeji), ambapo waliishia hatua ya makundi.
  • Hii ni mara ya tatu kwa Hungary kushiriki katika michuano hii, mara yao ya kwanza ilikuwa mwaka 1972. Moja ya perfomance zao nzuri za kukumbukwa katika michuano mikubwa ilikuwa ni pale walipowafunga mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia mwaka 1938 na 1954.
  • Katika awamu tatu za mwisho walizoshiriki katika michuano mikubwa, Austria wamekuwa wakitolewa katika hatua za makundi (Kombe la Dunia 1990 na 1998 pamoja na Euro 2008)
  • Katika michezo mitatu ya michuano ya Euro ambayo Austria waliyoshiriki mwaka 2008, yalipatikana magoli manne (walifunga moja, walifingwa matatu). na kutumia nafasi moja tu kati ya 46 walizopata.
  • Hungary ndio timu yenye tofauti ndogo ya magoli kufunga na kufungwa kati ya timu zote zilizofuzu katika michuano hii (+2, ukiondoa michezo ya mtoano (playoffs)).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here