Home Kimataifa TOP 10 YA WAFUNGAJI BORA ZAIDI KATIKA HISTORIA YA MICHUANO YA EURO

TOP 10 YA WAFUNGAJI BORA ZAIDI KATIKA HISTORIA YA MICHUANO YA EURO

4132
0
SHARE

 

Haya sasa ule muda umewadia tena, Mashindano ya Euro yanakaribia kuanza tena. Mashindano ya Euro yamebahatika kushirikisha Washambuliaji bora zaidi katika historia ya Soccer tangu yaanze mwaka 1960, mashabiki wengi watawasha luninga zao mwezi huu kushuhudia wakina Jamie Vardy, Thomas Muller, Cristiano Ronaldo na wengineo wakifanya yao lakini je unawajua wafungaji 10 bora zaidi katika historia ya michuano ya Euro katika msimu mmoja?

 1. Wayne Rooney

EuroWayne Rooney ni moja ya wachezaji waliopata mafanikio makubwa sana katika historia ya klabu yake ya Manchester United na hata timu yake ya taifa England. Kiwango chake alichoonesha katika michuano ya Euro 2004 iliyofanyika Ureno bado inamfanya akumbukwe kama mchezaji aliyeonesha uwezo mkubwa sana katika mashindano yake ya kwanza ya Euro.

Rooney alliweza kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga goli katika historia ya mashindano ya Euro pale alipoweza kuipiga timu ya Uswisi goli mbili. Rooney aliweza kumaliza mashindano hayo akiwa amefunga mara nne katika mechi nne alizocheza akiwa na miaka 18 tu, tukifananisha na mpira wa sasa ni sawasawa  na kijana Marcus Rashford aweze kupachika goli nne kule ufaransa, ama kweli Rooney alikuwa moto wa kuotea mbali.

 1. Savo Milosevic

Aston Villa vs Leeds Utd, 24/3/96, Coca Cola Cup final Pic : Brandon Malone / Action Images Aston Villa's Savo Milosevic scores Leeds United

Ninauhakika wengi wenu sasa hivi mtakuwa mnajiuliza huyu ni nani? Milosevic ni mchezaji mahiri alliyeweza kucheza soka miaka 16 katika nchi mbalimbali barani Ulaya, alicheza miaka mingi sana katika nchi za Uhispania na Uingereza. Milosevic aliweza kuichezea timu yake ya taifa ya Serbia mara 102, lakini katika mechi hizi 102 mechi  5 alizozicheza katika mashindano ya Euro 2000 ndizo zinazokumbukwa na mashabiki wengi ulimwenguni.

Milosevic aliweza kuifikisha timu yake robo fainali, jambo ambalo halikuwahi kutokea katika historia ya timu ya Serbia. Milosevic aliweza kufunga magoli matano katika mechi nne alizocheza na kwa kufanya hivyo aliweza kuchukua tuzo ya mfungaji bora ama Golden  Boot pamoja na Patrick Kluivert wa Uholanzi ambaye walilingana magoli katika mashindano hayo. Arsenal mtafuteni huyu labda bado anacheza.

 1. Nuno Gomes

Euro 2

Nuno Miguel Soares Pereira Ribeiro ni mchezaji ambaye alizaliwa na kipaji cha kufunga magoli, aliweza kufunga magoli mengi sana kwa ajili ya klabu yake na hata nchi yake. Katika mechi ya nne kwa ajili ya timu yake ya Ureno ambayo aliicheza katika michuano ya Euro 2000 nchini Uholanzi, aliweza kufunga goli lake la kwanza kwa timu ya Ureno na kama hiyo haitoshi alipachika mengine mawili katika mechi iliyofuata, alimaliza mashindano hayo akiwa na magoli manne katika mechi tatu na aliweza kuongeza mengine mawili katika michuano  ya Euro 2004 na Euro 2008.

 1. Cristiano Ronaldo

Euro 3

Sidhani kama kuna shabiki wa mpira asiyemjua huyu jamaa, kwa hiyo sitomuongelea sana. Siyo siri kwamba huyu jamaa ameweza kupata mafanikio mengi sana katika maisha yake ya mpira, lakini tofauti na wachezaji wengine katika hii list ambao waliweza kupachika mabao mengi katika mchuano mmoja yeye magoli yake ameyagawanya katika michuano tofauti tofauti. Aliweza kufunga mabao mengi zaidi katika michuano ya Euro 2008 ambayo alifunga mabao matatu, aliweza kufunga mabao mawili mwaka 2008 na hata kuiwezesha timu yake kufika fainali ya michuano hiyo iliyofanyika nyumbani kwao Ureno. Euro 2012 haikuwa nzuri kwake kwani alifunga bao moja tu.

 1. Thierry Henry

Euro 4

Huyu jamaa alikuwa hatari siyo kwa Arsenal tu bali hata nchi yake vilevile. Henry anakumbukwa kuwa moja ya washambuliaji wakali zaidi waliowahi kucheza mpira, anajulikana kama mfungaji bora zaidi kwa klabu yake ya Arsenal, huyu jamaa ana sanamu nje ya Emirates stadium, hilo tu linaonesha ukali wake.

Henry aliweza kuisadia timu yake kutwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 21 tu na katika mashindano yake ya Euro ya kwanza mwaka 2000, aliweza kufunga mara tatu na kuiwezesha Ufaransa kushinda michuano hiyo, katika  michuano yake ya pili mwaka 2004 aliweza kufunga mara mbili lakini timu yake haikufanikiwa kutetea ubingwa wao kwani walitolewa hatu ya robo fainali.

Alicheza michuano yake ya mwisho mwaka 2008 na alifunga bao pekee la timu yake katika michuano hiyo, cha kuchekesha ni kuwa kocha wake wa Juventus alikuwa anamchezesha Henry winga na hata beki siku nyingine kabla ya Arsene Wenger kuona kipaji chake na kumsajili.

 1. Zlatan Ibrahimovic

Euro 5

Mcheza Karate Zlatan Ibrahimovic ni moja ya washambuliaji bora zaidi duniani, ninauhakika mashabiki wa club ya Manchester United mnatamani sana jamaa huyu avae uzi wenu msimu ujao.

Zlatan anasifika kwa kufunga magoli ya ajabu sana kama unabisha angalia goli lake dhidi ya Ufaransa Euro 2012, ameweza kuicheza timu yake ya taifa ya Sweden katika mchuano mitatu ya Euro na ameweza kupachika magoli mawilimawili katika michuano yote hiyo, ni moja ya wachezaji watatu kwenye orodha hii ambao wanaweza kuongeza idadi yao ya magoli katika michuano ya euro 2016 lakini atahitaji usaidizi mkubwa kutoka kwa timu yake ili kufanikisha hili.

 1. Patrick Kluivert

Euro 6

Kluivert alikuwa moja ya wachezaji bora katika kizazi chake ila hakuweza kufanikiwa kucheza mpira kwa muda mrefu kutokana na majeruhi. Alishiriki katika michuano miwili  ya Euro. Akiwa na miaka 19 tu mshambuliaji huyu aliweza kushiriki michuano yake ya kwanza ya Euro ila kutokana na majeruhi alikosa mechi mbili za kwanza za timu yake, ila alifanikiwa kufunga goli katika mechi ya tatu na kuifikisha timu yake hatua ya mtoano.

Mnamo Euro 2000 aliweza kujitangaza duniani kama mmoja ya washambuliaji bora zaidi kwani alifunga magoli matano katika mechi tano katika mashindano hayo, na hata kuifikisha timu ya Uholanzi hatua ya nusu fainali.

 1. Ruud Van Nistelrooy

Euro 7

Van Nistelrooy ni mshambuliaji mwingine kutoka nchi ya Uholanzi. Huyu jamaa alizaliwa na uwezo wa kunusa magoli, kwani aliweza kufunga magoli mengi sana kwa kutumia uwezo wake wa kuvizia au poaching kwa ugha ya Kingereza. Japo aliweza kupata mafanikio mengi zaidi kushinda Kluivert ila nae alisumbuliwa sana na matatizo ya majeruhi.

Alianza vizuri sana katika michuano yake ya kwanza ya Euro mwaka 2004 kwani aliweza kufunga bao katika mechi zake tatu za kwanza na hatimaye alimaliza mashindano hayo akiwa na mabao manne, mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 32 aliweza kuongeza mabao mawili mengine katika idadi yake.

 1. Alan Shearer

Euro 8

Sidhani kama alishawahi kutokea mshambuliaji mzuri zaidi ya Shearer alipokuwa katika ubora wake. Alicheza michuano yake ya kwanza mwaka 92 lakini hakucheza sana na alishindwa kufunga goli katika mashindano hayo, lakini mnamo mwaka 96 alikuwa tayari kashajulikana kama moja ya wachezaji bora zaidi duniani na aliweza kufunga mabao matano katika mechi tano alizocheza katika michuano ya Euro ya mwaka huo.

Aliweza hata kuifikisha timu ya England nusu fainali ya michuano hiyo na yeye binafsi alipewa tuzo ya mfungaji bora katika Euro ya mwako huo. Euro 2000 ilikuwa mbaya kwa England kwani hawakufanikiwa hata kutoka hatua ya makundi ila Shearer aliweza kupachika magoli mawili katika mechi tatu alizocheza.

 1. Michel Platini

Euro 9

Platini ni moja ya viungo bora zaidi aliyewahi kutokea katika mpira, ukichunguza orodha hii vizuri utagundua kama wachezaji wote waliorodheshwa ni washambuliaji na walishiriki Euro zaidi ya moja ili kufikisha idadi yao ya Magoli, wote kasoro huyu jamaa.

Platini alishiriki Euro ya mwaka 84, alifanikiwa kufunga goli katika kila mechi aliyocheza na hata kupiga hat-trick katika mechi mbili mfululizo katika mashindano hayo, sidhani kama itamshangaza mtu kusikia kwamba aliiwezesha Ufaransa kushinda kombe hilo. Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane alinukuliwa akisema kwamba mechi ya nusu fainali ya Euro 84 kati ya Ufaransa na Ureno ambayo Platini alifunga bao la ushindi katika dakika za nyongeza ndiyo sababu iliyomfanya yeye kuanza kucheza mchezo wa mpira.

Hakuna mchezaji katika historia ya mpira ambaye atakuja kusogelea rekodi ya Michel Platini ya goli 9 katika mechi 5 kwenye michuano ya Euro, labda Messi ageuke kuwa Mwingereza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here