Home Kitaifa PICHA 6: MASHABIKI WA KEKO MACHUNGWA WALIVYOTISHA NDANI YA UZI WA NDONDO...

PICHA 6: MASHABIKI WA KEKO MACHUNGWA WALIVYOTISHA NDANI YA UZI WA NDONDO CUP 2016

644
0
SHARE

Keko Machungwa

Michuano ya Sports Extra Ndondo Cup inayodhaminiwa na Dr. Mwaka na kurushwa live na kituo cha television cha Azam TV kupitia channel zake za Azam Sports HD na Azam Two.

Jumapili ya June 5, utafanyika uzinduzi rasmi wa hatua ya makundi ambapo timu 32 zitachuana katika hatua hiyo kutafuta timu 16 zitakazofuzu kwa ajili ya hatua ya mtoano.

Temeke Market kutoka mitaa ya Temeke, watachuana na mabingwa watetezi wa taji hilo timu ya Faru Jeuri kutoka kitaa cha Vingunguti kwenye mechi ya ufunguzi wa hatua ya makundi.

Kuelekea siku ya uzinduzi wa michuano hiyo, mashabiki wa Keko Machungwa wamepiga picha kali sana na kunitumia kwenye email yangu, kutokana na ukali la ubora wa picha hizo, nimeamua kuwapa ‘shavu’ kwa kuzipandisha mtandaoni ili wadau wengine wa Ndondo Cup pamoja na mashabiki wa timu mbalimbali wazishuhudie.

Hii ni fursa na kwako pia, kikundi cha mashabiki wa timu zinazoshiriki michuano ya Ndondo kupiga picha kali ukiwa ndani ya jezi au T-shirts za timu unayoishabikia ikiwa ni pamoja na selfie halafu zitume kwangu na mimi bila ajili nitazipandisha mtandaoni ili ku-share na wadau wengine kote ulimwenguni.

Tuma picha kupitia email hii masanjadickson@gmail.com, kisha usubiri kuziona kwenye mtandao wako wa shaffihdauda.co.tz unaokuweka karibu na stori zote kali za michezo saa 24 kila siku za wiki.

Cheki picha za mashabiki wa Keko Machungwa wakiwa wamependeza ndani ya jezi za timu yao 

IMG_20160602_114455 IMG_20160602_114513 IMG_20160602_103021 IMG_20160602_103312 IMG_20160602_102903 IMG_20160602_103521

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here