Home Kimataifa FAINALI ZA NBA, GOLDEN STATE WARRIORS YAICHAPA CAVALIERS MCHEZO WA KWANZA.

FAINALI ZA NBA, GOLDEN STATE WARRIORS YAICHAPA CAVALIERS MCHEZO WA KWANZA.

1227
0
SHARE

finals

Hii ni fainali ya sita mfululizo mchezaji wa klabu ya Cleveland Cvaliers, Lebron James au maarufu kama King James anacheza. Ameweka rekodi ya kuingia kwenye kila orodha ya kila  kumi bora ya utoaji pasi, kufunga pointi nyingi, kudaka rebound na kupokonya mipira katika hatua ya mtoano ya NBA yaani post season.

Fainali ya mwaka huu ni marudio ya fainali zilizopita ambapo Golden State Warriors walitwaa ubingwa huku Lebron akiwa anacheza bila wachezaji wawili muhimu ambao ndio hukamilisha ile Big Three ya Cavs ambao ni Kyrie Irving aliyeumia mchezo wa kwanza wa fainali hizo na Kevin Love aliyekuwa kaumia wakati msimu ukiendelea.

Stephen Curry na Golden State Warriors walipitia njia ambayo wengi waliamini walikuwa wameshaondolewa baada ya kuwa nyuma kwa michezo 3-1 dhidi ya Oklahoma City Thunder. Kabla ya kutoka nyumba na kuibuka na ushindi wa michezo 4-3 huku Lebron na Cavs wakiifumua Toronto Raptors 4-2 katika fainali ya Mashariki.

Katika mchezo wa kwanza Alfajiri ya leo Warriors wameibuka na ushindi wa vikapu 89-104. Tofauti na ilivyozoeleka sio Stephen Curry wala Klay Thompson ambao ndio wachezaji wanaoongoza kufunga pointi nyngi zaidi katika kikosi cha Warriors waliokuwa vinara wa pointi leo.

Curry alikuwa na usiku mbovu kwani alipata mitupo 4 peke yake kati ya 15 na kumaliza na pointi 11, huku Klay Thompson akimaliza na pointi 9 na kufanya watu hawa kupata jumla ya pointi 20 pekee kwa mitupo 27.Lilikuwa ni benchi la Warriors lililoleta tofauti kwani mchezaji Shaun Livingston alifunga pointi zake nyingi zaidi katika maisha yake ya mpira wa kikapu katika kipindi cha mtoano.

Shaun Livingston akifunga moja ya vikapu vyake mbele ya Mathew Dellavedova, Iman Shumpert na Kevin Love
Shaun Livingston akifunga moja ya vikapu vyake mbele ya Mathew Dellavedova, Iman Shumpert na Kevin Love

Shaun Livingston alimaliza na pointi 20, huku benchi la Warriors likifunga zaidi ya pointi 50. Iguodala aliongeza 12, Green alifunga 16, Harrison Barnes aliyeanza mchezo kwa kumkaba Lebron alifunga 13, Leandro Barbosa akapata mitupo yote 5 aliyojaribu na kufunga pointi 11 huku Andrew Bogut akimaliza na pointi 10.

Kwa upande wa Cavaliers, Mchezaji Lebron James alimaliza mchezo akiwa na pointi 23 huku akipata mitupo 9 kati ya 21 aliyojaribu. Kyrie Irving alimaliza mchezo na pointi 26 huku Kevin Love akifunga pointi 17.

Hii inamaanisha kuwa Big Three wa Cavs walifunga pointi 66 dhidi ya 36 za Big Three wa Warriors. Lakini wachezaji wa benchi ndio walioleta tofauti kwa kufunga wachezaji wa Warriors kufunga pointi 45 dhidi ya 10 za benchi la Cavs.

HISTORIA.

Lebron James sasa ana rekodi ya kutokushinda mchezo wowote wa kwanza wa fainali usipochezwa katika uwanja wa nyumbani yaani timu yake ikikosa hoe court advantage. Ana rekodi ya 0-5.

Warriors wana rekodi ya kushinda 6-2 katika michezo ya ufunguzi ya fainali za NBA.

Timu zilizofanikiwa kushinda michezo zaidi ya 65 ya msimu zina rekodi ya kushinda mara 13 katika Fainali huku zikipoteza mara 2 pekee.

Timu zinazokuwa na MVP wa ligi zina rekodi ya kushinda mara 19 katika fainali huku zikipoteza mara 7 pekee.

Timu zilizoshinda mchezo wa kwanza wa Fainali zimekuwa na rekodi ya kuwa na asilimia 79 ya kutwaa ubingwa wa NBA.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here