Home Kimataifa UCHAMBUZI WA KUNDI LA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

UCHAMBUZI WA KUNDI LA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

1648
0
SHARE

Yanga-conf

Na Athumani Adam

Baada ya kuiondoa Sagrada Esperanca ya Dundo nchini Angola kwenye hatua ya kumi na sita bora, mashindano ya shirikisho barani Afrika wapenzi wa soka nchini Tanzania shauku yao kubwa ilikua kuona kundi ambalo Yanga itapangiwa. Siku zikaenda, hatimae Jumanne May 24 droo ikafanyika kule jijini Cairo ndipo Yanga ambayo imetinga hatua kubwa ya makundi kwenye michuano ya Afrika baada ya miaka kumi na nane kupita ikaangukia kundi A.

Timu nyingine kwenye kundi hilo ni Mo Bejaia kutoka Algeria, Medeama ya Ghana pamoja na TP Mazembe ya Jamuhuri ya Congo. Baada ya upangaji wa makaundi stori kubwa imekuwa ni kuhusu TP Mazembe huku timu za Mo Bejaia na Medeama haziongelewi sana kwenye vinywa vya wapenda soka nchini. Kuelekea michezo ambayo itaanza katikati ya mwezi June makala hii inakupa uchambuzi juu ya kundi hili kwa kuziangalia timu ambazo zimepangwa na Yanga.

Mo Bejaia (Algeria)

Inajulikana kama Moulodia Olympique de Bejaia, inatoka katika mji wa Bejaia nchini Algeria. Imetinga kwenye hatua ya makundi kwa kuwaondoa Esperance ya Tunisia ambayo iliondoa timu ya Azam kutoka hapa nyumbani Tanzania.

Mo Bejaia ilitoka suluhu na Esperance nyumbani 0-0 na kwenye mechi ya marudiano kule Tunisia wakapata sare ya 1-1 na kuvuka kwa sheria ya goli la ugenini. Tangu Mo Bejaia ilipoanzishwa mwaka 1954, wana taji moja tu la kitaifa ambalo ni kombe la Algeria (Algeria Cup) pia mwaka 2010/11 walishinda ubingwa wa ligi kwa kanda ya Mashariki.

Kwenye kikosi chao cha sasa wana wachezaji wa kigeni watatu, pia wanashika nafasi ya tano kwenye ligi na timu kumi na sita nyuma ya timu za Usm Alger, Js Saoura, Js Kabylie na Es Setif timu ambayo ilifungwa na Simba miaka 4 iliyopita kwenye kombe hili.

Mo Bejaia itakutana na Yanga tarehe 17/6/2016 kule Algeria na kurudiana 12/8/2016 Dar es salaam

Medeama (Ghana)

Kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm aliwahi kufanya kazi Ghana kwenye timu ya Berekum Chelsea, hivyo bila shaka anaifahamu vizuri timu hii. Medeama ilianzishwa mwaka 2002 kwenye mji wa Tarkwa kule Ghana ikijulikana kwa jina la Kessben FC kabla ya kubadili jina mwaka 2011.

Medeama haijawahi kuchukua ubingwa wa Ghana Plo League lakini wana vikombe viwili vya FA mwaka 2013 na 2015. Pia wana ubingwa wa Super Cup 2015.

Kwenye hatua iliyopita ya kombe la shirikisho walipita kwa goli la ugenini baada ya ushindi wa 2-0 nyumbani na kupoteza 3-1 ugenini dhidi ya Mamelodi Sundown. Sundown licha ya kutolewa imejikuta na bahati kwa kurudi tena kwenye klabu bingwa kutokana na As Vita ambayo iliitoa Sundowns kwenye klabu bingwa kumtumia mchezaji mwenye adhabu Idrissa Traore ambaye wamemsajili msimu huu kutoka Stade Malien ya Mali.

Kwenye kikosi chao cha sasa hawana mchezaji yeyote raia wa kigeni. Kwenye ligi ya Ghana timu hii ipo nafasi ya 9 kati ya timu 16 baada ya michezo 15 kufanyika

Yanga itaanza nyumbani dhidi ya Medeama tarehe 15/7/2016 kabla ya kwenda ugenini nchini Ghana tarehe 26/7/2016

TP Mazembe (DR CONGO)

Mazembe wamefika hatua hii kwa kuiondoa Stade Gabasien kwa goli la ugenini baada ya ushindi wa 1-0 nyumbani kasha kupoteza ugenini 2-1. Mazembe yenye makao makuu jijini Lumbumbashi ni timu yenye mafanikio kwa bara la Afrika. Ni timu ambayo imewahi kucheza fainali nne mfululizo za klabu bingwa Afrika.

Pia ni timu ya kwanza kutetea ubingwa wa klabu bingwa Afrika kabla ya Enyimba kuvunja rekodi yao mwaka 2003 na 2004. Wamefika fainali ya klabu bingwa dunia mwaka 2010 kisha kupoteza fainali dhidi ya Intermilan chini ya Rafael Benitez.

Mazembe tangu kuanzishwa mwaka 1939 wametwaa vikombe 14 vya ligi, 5 Copa du Congo, 5 Super Copa du Congo, 5 klabu bingwa Afrika, 1 kombe la washindi Afrika na 3 CAF Super Cup
Tangu mwaka 1997 ipo chini ya Rais Moise Katumbi kwenye kikosi cha sasa wana wageni 17 kutoka mataifa ya Tanzania, Ivory Coast, Zambia, Ghana na Mali

Yanga itaanza nyumbani dhidi ya Mazembe tarehe 28/6/2016 na baadaye kwenda kurudiana jijini Lubumbashi nchini Congo tarehe 23/8/2016

Kwa majadiliano zaidi,  tuwasiliane kupitia; Facebook: Athumani Adam, Email: Athumani46664@gmail.com

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here