Home Ligi EPL Monchi: Miaka 16 na Sevilla, Makombe 9, £150m ya faida – muda...

Monchi: Miaka 16 na Sevilla, Makombe 9, £150m ya faida – muda umefika kwenda kumsaidia Mourinho Old Trafford 

774
0
SHARE

Mkurugenzi wa michezo wa Sevilla, Monchi ameomba kuondoka kwenye klabu hiyo huku akiripotiwa kuwa mbioni kwenda kufanya kazi EPL.

  Tottenham na Liverpool wameshajaribu kumuajiri mhispaniola huyo ‘Mr Moneyball’ huko nyuma lakini hivi sasa anahusishwa na kujiunga na kikosi cha Jose Mourinho katika kumsaidia kwenye masuala ya uhamisho.
Monchi, mwenye umri wa miaka 47 amesaidia kuiongoza Sevilla kushinda makombe 9 katika miaka 10 na kutengeneza faida ya  €200m (£152m) katika soko la uhamisho.

Katika mahojiano aliyofanya na gazeti la Dailymail la Uingereza mnamo mwezi uliopita, Monchi ambaye jina lake hakisi ni: Ramon Rodriguez Verdejo – alisema ingawa aliwahi kutumia miezi 6 kuishi nchini UK katika msimu wa 2013-14 lakini ilikuwa ni kwa ajili ya kujifunza kiingereza ili aweze kujiongezea ufanisi katika kufanya kazi yake akiwa na Sevilla na sio kutengeneza mazingira ya kuhamia England. Hata hivyo, baada ya kutofautiana na maofisa wakuu zaidi yake wa Sevilla, aliamua kusitisha interview jumapili usiku iliyokuwa imepangwa na klabu.
Sevilla jana walithibitisha kwamba golikipa huyo wa zamani wa klabu aliomba kuondoka kwa sababu binafsi lakini wamemwambia kuna kiasi cha fedha inabidi alipe ili aweze kuvunja mkataba. Klabu hiyo imesema bado inahitaji huduma za Monchi na wasingependa aondoke.

 Monchi alianza kufanya kazi na Sevilla wakati klabu hiyo ikiwa katika ligi daraja la pili nchini Spain, miaka 16 iliyopita wakati klabu ikiwa inakaribia kufilisika. Kidogo kidogo, msimu kwa msimu, Sevilla walitumia £11.65m kumsajili Ivan Rakitic, Dani Alves, Julio Baptista, Federico Fazio, Gary Medel, Seydou Keita na Geoffrey Kondogbia. Wakaanza kupata mafanikio.

Mafanikio hayo yalipelekea kuuzwa kwa timu hiyo kwa kiasi cha £145m. Katika kipindi hiki Sevilla wakafanikiwa kushinda makombe 9 yakiwemo matano ya Europa League na moja la Supercup huku wakitengeneza faida ya  £160m kutoka na biashara ya uhamisho. Monchi anaeleza siri ya mafanikio: “Huwa tunanunua wachezaji wakati wakiwa hawafahamiki lakini wakiwa wanaelekea kwenye kilele cha ubora wa vipaji vyao, baada ya hapo tunawauza wakishakuwa maarufu na vipaji vyao vikiwa vimeimarika. Tuna mlengo wa kutengeneza faida huku tukipata matokeo chanya uwanjani.”

 Kwanini United wanatajwa kumhitaji? 

Ukiangalia namna United walivyotumia fedha nyingi katika usajili katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, wachambuzo wa mambo wanasema Mourinho atahitaji usaidizi wa Mkurugenzi wa ufundi katika jitihada za kuirudisha United kileleni tena.

Anaweza kuwa mmoja wa makocha bora duniani kwa sasa lakini bado kwenye dirisha la usajili hayupo fiti vya kutosha. Monchi anaweza kuwa msaada kwake. “Mimi huwa ni msaidizi mzuri wa kocha, mwalimu ananipa ananipa maeleo ya mchezaji anayemtaka halafu mimi na timu yangu ya scouting tunaanza kazi. Maelewano ya kikazi na mwalimu ni kitu muhimu sana.” – alisema Monchi
Kufanya kazi pembeni ya Mourinho ni kitu kinachohitaji kujiongeza kwa 100%, na kutokana sera na utamaduni wa Man United wa kukuza soka la makinda, Monchi atakuwa msaada mkubwa kwa Special One.

Katika kipindi cha miaka 16  akiwa Sevilla, Monchi alifanikiwa kuwaibua makinda kama Sergio Ramos, José Antonio Reyes, Aleix Vidal, Jesús Navas na Alberto Moreno. Lakini hakusita kupokea ofa watu walipofika madau makubwa. Aliwauza, akifuata sera yake katika soka ya kuwapa nafasi makinda, kushinda mechi, kuwasaidia makinda kufikia katika ubora wao, kisha kuwauza huku akiendelwa kushinda mechi.

Hivi sasa wakiwa na wachezaji makonda kama Marcus Rashford na Timothy Fosu-Mensah ambao wanang’ara na kurudisha heshima ya United katika kuwa na academy bora. Kumuongeza Monchi kutasaidia katika kuwaongoza wachezaji hao kwenye mafanikio.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here