Home Kimataifa TWEET YA GOTZE YAZUA GUMZO BAADA YA REUS KUTEMWA KIKOSI CHA UJERUMANI

TWEET YA GOTZE YAZUA GUMZO BAADA YA REUS KUTEMWA KIKOSI CHA UJERUMANI

873
0
SHARE

Reus-Gotze

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low amemwacha nyota wa Borussia Dortmund Marco Reus kwenye kikosi cha wachezaji 23 kitakacholiwakilisha taifa hilo kwenye michuano ya EURO mwaka huu itakayofanyika nchini Ufaransa.

Reus alikosa michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 kutokana na majeraha.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Low amesema: “Yamekuwa ni maamuzi yaliyotuumiza sisi na yeye (Reus), na yenye fedheha kwetu”.

“Marco Reus ambaye yuko fiti kwa asilimia mia moja angekuwa ni hazina kubwa sana kwetu”.

“Nawashukuru sana wachezaji hawa wanne, walijitahidi sana mazoezini, walijitolea kwa nguvu zao zote na ni matumaini yangu kwamba hawatofedheheshwa na jambo hili”.

Haya hayakuwa maamuzi dhidi ya wachezaji wanne bali yamekuwa ni maaamuzi kwa ajili ya wachezaji 23”.

Ikumbukwe tu leo ilikuwa ni birthday ya Reus na rafiki yake Mario Gotze ali-tweet kwenye twitter yake akisema: “Hongereza @Marco kwa siku yako ya kuzaliwa, nasubiri kwa hamu kuwa pamoja nawe katika michuano ijayo ya EURO”.

Sasa baada ya kuona jina la rafiki yake kipenzi halipo kwenye timu ya taifa, ghafla akaifuta tweet hiyo na kuandika “Hongera kwa siku ya kuzaliwa @Marcihno11 lakini tuna huzuni kubwa. Siamini. Nimeumia sana.

 

Kikosi kilichotangazwa kuiwakilisha Ujerumani ni pamoja na;

Magolikipa: Manuel Neuer (Bayern Munich), Bernd Leno (Bayer Leverkusen), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona).

Walinzi: Jerome Boateng (Bayern Munich), Emre Can (Liverpool), Jonas Hector (Cologne), Benedikt Howedes (Schalke), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Shkodran Mustafi (Valencia), Antonio Rudiger (Roma).

Viungo: Julian Draxler (Wolfsburg), Mario Gotze (Bayern Munich), Sami Khedira (Juventus), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Toni Kroos (Real Madrid), Mesut Ozil (Arsenal), Leroy Sane (Schalke), Bastian Schweinsteiger (Manchester United), Julian Weigl (Borussia Dortmund).

Washambuliaji: Mario Gomez (Besiktas), Thomas Muller (Bayern Munich), Lukas Podolski (Galatasaray), Andre Schurrle (Wolfsburg).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here