Home Kitaifa TAMBWE, NGOMA, WAMKIMBIZA NONGA YANGA

TAMBWE, NGOMA, WAMKIMBIZA NONGA YANGA

781
0
SHARE

Yanga v Mlale 1

Na Yahaya Mohamedy

Mshambuliaji wa klabu ya Young Africans Paul Nonga ameamua kuomba kuachana na timu hiyo baada kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Nonga ameuambia mtandao huu kwamba, uamuzi huo wa kuandika barua kuomba kuuzwa utaisaidia klabu hiyo kutopata hasara.

”Nimeomba kuuzwa na tayari barua ipo mezani kwenye ofisi ya Yanga na nimewatajia mahali ninapopenda kuuzwa, nimeomba kuuzwa ili wasiingie hasara kwasababu walininunua kwa pesa nyingi. Sababu kubwa ya maamuzi Yangu haya ni nafasi finyu ya kucheza niliyonayo katika kikosi cha Yanga kutokana ubora walionao wenzangu wanaocheza nafasi niichezayo na wanatimiza majukumu yao ipasavyo na kuitendea haki nafasi hiyo”, amesema Nonga.

Nonga ameongeza kuwa uamuzi huo ni wakwake mwenyewe na wala hajashurutishwa, ”Maamuzi haya ni yangu binafsi sijashurutishwa na mt, nafanya hivi ili nijaribu kukinusuru kipaji changu”, aliongeza.

Nonga alinunuliwa katikati ya msimu uliopita akitokea Mwadui FC kwa kiwango cha fedha ambacho hakikuwekwa wazi.

Changamoto ya nafasi ya Nonga kucheza katika kikosi cha kwanza ni kutokana na kusheheni kwa wachezaji wenye uwezo mkubwa katika nafasi yake.

Wachezaji walio katika nafasi hiyo ni Amisi Tambwe ambaye ndiye mfungaji bora akiwa na magoli 21 , Donald Ngoma mwenye magoli 17.

Washambuliaji wengine ni Malimi Musungu na Matheo Anthon.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here