Home Kimataifa #UCL: Zinedine Zidane kufuata nyayo za Guardiola kwa kuwa kocha wa 8...

#UCL: Zinedine Zidane kufuata nyayo za Guardiola kwa kuwa kocha wa 8 kutwaa Champions League katika msimu wa kwanza?

900
0
SHARE

Zinédine Zidane aliteuliwa kuwa kocha wa Real Madrid mapema mwezi January 2016 – lakini anaweza kuingia kwenye historia soka wiki hii kwa kuwa mmoja wa makocha waliobeba ubingwa wa Champions League katika msimu wake wa kwanza.

image

Zidane tayari alimshaisaidia kazi Carlo Ancelotti alipokuwa Madrid na akawa kocha wa kikosi cha reserve kabla ya kupandishwa cheo baada ya kuondoka kwa Rafa Benitez. Baada ya kuiongoza Madrid katika hatua tatu za mtoano mpaka kufikia fainali ya Jumamosi vs Atletico, Zidane huenda akafuata nyayo za makocha bora kuwahi kutokea kwenye michuano hii.

image

1. 1956: José Villalonga (Real Madrid)
Huyu alibeba ubingwa wa ulaya katika msimu wake wa kwanza – msimu ambao kombe hili ndio lilikuwa linashindaniwa kwa mara ya kwanza. ‘Pepe’ Villalonga tayari alishakuwa kocha wa Madrid tangu kuanzia msimu wa 1954/55, alishinda ubingwa wa ligi na akafanikisha kushinda kombe la ulaya. Baada ya hapo alihamia Atletico mwaka uliofuatia na alifanikiwa kwenda kuwafunga Madrid katika fainali ya Copa kisha kwenda kushinda ubingwa wa kombe la washindi la ulaya mnamo mwaka 1962. Villalonga alifariki dunia mwaka 1973 akiwa na miaka 53.

image

2. 1960: Miguel Muñoz (Real Madrid)
Nahodha wa kikosi cha Villalonga kilichoshinda ubingwa mwaka 1956 na 1957 alistaafu soka na kuwa kocha. Munoz alichukua majukumu ya benchi la ufundi la Real Madrid msimu wa 1959/10 na timu tayari ilishafika nusu fainali – na yeye kama Zidane alianza kwa kuwafundisha reserves. Madrid tayari walikuwa wameshashinda makombe manne ya ulaya na ujio wa Munoz ukaleta kombe la 5 – nusu fainali wakiwafunga wapinzani wao FC Barcelona 3-1 nyumbani na Ugenini na kisha wakaenda kuwafunga Eintracht Frankfurt 7-3 katika fainali maarufu iliyotazamwa na watu 127,621. Mpaka muda anaondoka Madrid tayari walishashinda kombe lingine la ulaya mwaka 1966 na makombe 9 ya La Liga.

image

3. 1982: Tony Barton (Aston Villa)
Winga wa zamani wa vilabu vya Fulham, Nottingham Forest na Portsmouth katika miaka ya 1950 – 1960. Barton alikuwa miongoni mwa makocha wa benchi la ufundi katika klabu ya Aston Villa wakati kocha mkuu Ron Saunders alipojiuzulu mnamo February 1982. Wakiwa tayari kwenye robo fainali, Barton akaiongoza Villa mpaka kwenda kushika ubingwa wao wa ulaya – akiwafunga Dynamo Kyiv na Anderlecht bila kuruhusu wavu wao kuguswa katika hatua ya robo na nusu fainali. Hatua ya mwisho wakakutana na Bayern Munich jijini Rotterdam. Dakika 10 baada ya mchezo golikipa Jimmy Rimmer aliumizwa na Barton akamtoa na kumuingiza Nigel Spink ambaye alicheza mechi yake ya pili katika kikosi cha kwanza usiku huo na hakumuangusha kocha wake alipafomu vizuri na kuzuia michomo ya Bayern ambao waliishia kufungwa 1-0.

image

4. 1984: Joe Fagan (Liverpool)
Fagan aliteuliwa kuwa kocha mrithi wa mshindi wa mara 3 wa kombe la ulaya Bob Paisley katika klabu ya Liverpool mwaka 1983. Alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Liverpool tangu 1958 na huko nyuma alishawahi kuwa msaidizi wa kocha katika klabu ya Rochdale na kocha mchezaji katika timu Nelson ambapo alifanikiwa kushinda taji la Lancashire Combination katika msimu wake wa kwanza. Katika msimu wake wa kwanza kama kocha mkuu wa Liverpool msimu wa 1983/84, alifanikiwa kuiongoza Liver kushinda Ligi, League Cup na  European Cup, akiwafunga Roma katika fainali kwenye uwanja wa  Stadio Olimpico kwa penati.

image

5. 1988: Guus Hiddink (PSV Eindhoven)
Hiddink aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa PSV mnamo March 1987, akiwa tayari huko nyuma alikuwa msaidizi wa Hans Kraay ambaye alijiuzulu kufuatia kutokuwa na maelewano na uongozi wa klabu. PSV walikuwa wanaelekea kuchukua ubingwa wao wa pili mfululizo wa Eredivisie, Hiddink akapewa majukumu na kufanikiwa kuipa ubingwa wa ulaya kwa kuifunga Benfica kwenye mikwaju ya penati na kufanikiwa kufuata nyayo za mafanikio za wapinzani wao AJAX na Feyenoord. Tangu wakati huo Hiddink hajawahi kubeba tena kombe hilo.

image

6. 2000: Vicente del Bosque (Real Madrid)
Kocha wa kwanza kushinda kombe la UEFA Champions League katika msimu wake wa kwanza. Del Bosque alikuwa na historia sawa na Barton na Fagan – kabla ya mafanikio hawakuwa makocha wakubwa. Alishawahi kushinda ubingwa wa La Liga mara 5 akiwa mchezaji wa Madrid, baada ya hapo alikuwa msaidizi katika benchi la ufundi la Real, na mwaka 1994 alipata nafasi ya kushika hatamu kwa muda kabla ya John Toshack kuchukua majukumu ya benchi la ufundi la Los Blancos – aliendelea kumsaidia Toshack mpaka alipomrithi rasmi November 1999.  Madrid tayari walikuwa wameshavuka hatua ya makundi ya UCL na Del Bosque akaiongoza timu mpaka kufika fainali jijini Paris kucheza vs Valencia na wakashinda. Nsimu uliofuatia wakachukua La Liga, kabla Zizzou na galaticos wengine kuja kumsaidia kubeba ubingwa wake wa pili wa ulaya msimu wa 2001/02. Del Bosque alifukuzwa Madrid na baada ya muda akapata kazi katika timu ya taifa ya Spain na huko akafanikiwa kushinda ubingwa wa dunia na ulaya.

image

7. 2009: Josep Guardiola (Barcelona)
Miaka 53 baada ya maajabu ya Pepe Villalonga kupata mafanikio na Madrid katika msimh wake wa kwanza – Pep Guardiola nae akafanya hivyo na Barcelona. Mchezaji wa Barca katika kikosi cha ushindi wa kombe la ulaya mwaka 1992, alistaafu soka 2006 na mara moja akapewa nafasi ya kuiongoza Barcelona B. Miezi 11 baadae akamrithi Frank Rijkaard katika kikosi cha kwanza na kufabya mabadiliko makubwa yakiwemo kusajili wachezaji kama Dani Alves na Gerard Pique na kumleta Sergio Busquets na Pedro katika kikosi cha kwanza. Matokeo yake Guardiola akashinda makombe mawili nyumbani na kombe la UEFA Champions League.

Miaka 7 baadae keshokutwa jumamosi, mshindi wa kombe la UEFA Champions League Zinedine Zidane nae atakuwa anaiongoza klabu yake ya Real Madrid katika mchezo wa fainali vs Atletico Madrid – ikiwa ni miezi mitano tu tangu apewe majukumu. Je atafanikiwa kuwa kocha wa 8 kushinda Champions League katika msimu wake wa kwanza?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here