Home Kimataifa KUELEKEA DRAW YA MAKUNDI MICHUANO YA AFRIKA, CAF YAIPIGA CHINI CLUB MOJA...

KUELEKEA DRAW YA MAKUNDI MICHUANO YA AFRIKA, CAF YAIPIGA CHINI CLUB MOJA YA CONGO DR

568
0
SHARE

CAF

Kamati ya mashindano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambayo imekutana leo May 24 kusikiliza malalamiko ya klabu ya Stade Malien ya Bamako (Mali) juu ya klabu ya AS Vita Club ya Kinshasa (DR Congo) kumchezesha mchezaji Idrissa Traoré katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika kinyume na taratibu.

Idrissa Traoré alikuwa akiichezea Stade Malien mwaka jana. Na wakati akiichezea timu hiyo alishawahi kupata adhabu ya kufungiwa michezo minne na Kamati ya Nidhamu ya CAF. Lakini mchezaji huyo aliitumikia adhabu hiyo kwa mchezo mmoja tu na hivyo kubakiwa na adhabu ya michezo mitatu.

Kifungu 114.1 na 114.2 kanuni za CAF ndio kinatoa mwongozo wa adhabu inayomkabdili mchezaji huyo.

Hata hivyo, AS Vita iliamua kumchezesha mchezaji huyo katika hatua za awali za mtoano za michuano ya CAF hususan katika mchezo dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar uliopigwa February 2016.

Kutokana na kosa hilo, kwa kutumia kifungu cha 9 na 10 kinachopatikana katika Sura ya VII katika kitabu cha kanuni za michuano ya klabu bingwa Afrika, kamati ya nidhamu na mashindano ya CAF imeamua kuiondoa klabu ya AS Vita ya Kinshasa (DRC) katika michuano ya CAF Champions League mwaka huu, na nafasi yao kuchukuliwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, ambayo ndio walikuwa wa mwisho  kucheza na AS Vita kabla ya kuingia katika hatua ya makundi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here