Home Kitaifa MR. FREE-KICK ALIYEZIUA YANGA, AZAM, ATOA KAULI YAKE YA MWISHO COASTAL UNION

MR. FREE-KICK ALIYEZIUA YANGA, AZAM, ATOA KAULI YAKE YA MWISHO COASTAL UNION

695
0
SHARE

Miraji Adam

Mlinzi wa Simba SC Miraji Adam aliyekuwa anacheza kwa mkopo kwenye klabu ya Coastal Union ameandika ujumbe kupitia account yake ya facebook kuwaaga mashabiki wa Coastal Union mara baada ya mchezo wa mwisho wa ligi kati ya Coastal Union dhidi ya Tanzania Prisons.

Adam anawaaga mashabiki wa Coastal baada ya muda wake kuichezea klabu hiyo kumalizika lakini ameonesha masikitiko makubwa kutokana na timu hiyo kushuka daraja. Beki huyo ambaye alipata umaarufu kutokana na kuzifunga Yanga na Azam kwa free-kick kwenye mechi za VPL ambazo timu hizo zilipoteza kwa mara ya kwanza mechi zao za ligi dhidi ya Coastal.

Licha ya kumaliza muda wake wa kucheza kwa mkopo ndani ya timu hiyo ya Tanga ambayo imeshuka daraja, Miraji anasema yeye kwa sasa ni mchezaji huru.

“Napenda kuchkua fursa hii kuwa shukuru viongozi, mashabiki, wachezaji wote wa Coastal Union kwa support yenu mliyonipa kwa kipindi chote nilichokuwa na nyie katika timu yenu.”

“Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu wote ili kuisaidia timu ipate matokeo mazuri ila sikuweza kutimiza malengo hayo kwa asilimia zote na naamini hakuna mchezaji aliyependa timu kuwa hapo ilipo kila mtu anaumia, napenda kuomba radhi kwa mashabiki wote wa Coastal Union kama kuna kitu chochote niliwakosea au kama kuna mtu yoyote alinikosea basi nimemesamehe.”

“Pia naomba kuwashkuru mashabiki wote waliokuwa wananipa support kwa muda wote…nawapenda sana na nitazidi kuwakumbuka kwa mazuri yote mliyo nifanyia….ntawa-miss sana na nataka mjue kuanzia sasa mimi ni mchezaji huru….thanks Allah for everything”, amemaliza Miraji.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here