Home Kitaifa MGOSI, BARTHEZ, NGOMA DROO KUTIKISA NYAVU VPL

MGOSI, BARTHEZ, NGOMA DROO KUTIKISA NYAVU VPL

556
0
SHARE

IMG-20160522-WA0008

Musa Hassan Mgosi amefunga goli lake la kwanza kwenye msimu wa ligi ya Vodacom Tanzania bara ambao umehitishwa leo kwa timu zote kushuka viwanjani kukamilisha ligi.

Mgosi ambaye alisajiliwa na klabu ya Simba akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro ambako alifanya vizuri akiwa na wakatamiwa hao wa Manungu, Turiani.

IMG-20160522-WA0011

Tangu atue Simba kwa mara nyingine, Mgosi amekuwa hapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza Simba huku akitokea benchi kwenye baadhi ya mechi.

Nyota huyo wa zamani wa Stars leo amefunga bao moja likiwa ni bao lake pekee kwenye ligi msimu huu tangu arejee tena mtaa wa Msimbazi. Mgosi amefunga goli hilo dakika ya 70 kipindi cha pili wakati Simba ikipambana kusawazisha magoli ya Ruvu JKT iliyoibuka kidedea mbele ya Simba kwa kutandika magoli 2-1.

Mgosi na Ally Mustafa ‘Barthez’ ambaye pia leo alifunga goli lake la kwanza kwenye kwenye msimu huu, Barthez alifunga goli hilo kwa mkwaju wa penati na kuisawazishia Yanga iliyotoka sare ya kufungana bao 2-2 na Majimaji ya Songea.

Ushindi huo kwa Ruvu ulikuwa ni muhimu kwsababu walikuwa wakipambana kukwepa kushuka daraja na baadaye wamefanikiwa katika hilo na kuliacha janga hilo likiwaangukia African Sports, Coastal Union pamoja na Mgambo JKT zote zikiwa ni timu za mkoa wa Tanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here