Home Kitaifa MBEYA CITY: TUNAKAMILISHA MSIMU KWA ‘KUIUA’ NDANDA FC

MBEYA CITY: TUNAKAMILISHA MSIMU KWA ‘KUIUA’ NDANDA FC

602
0
SHARE

Mbeya City-Mbeya

KIKOSI cha Mbeya City Fc  kesho jumapili kinashuka kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa kucheza mchezo wa kufungia msimu  wa 2015/16 katika ligi kuu ya soka Tanzania  bara dhidi ya wageni Ndanda Fc kutoka mkoani Mtwara.

Muda  mfupi uliopita meneja  wa kikosi cha City, Geoffrey Katepa  ameidokeza mbeyacityfc.com kuwa  nyota wote 18 walitayrishwa kwa ajaili ya kuwakilisha  timu yao wako kwenye hari nzuri na tayari kabisa kusaka ushindi mbeya ya timu hiyo kutoka kusini mwa Tanzania.

DSC_0101

“Kama unavyoona  tumemaliza mazoezi  muda huu, yalikuwa ni mazoezi mepesi kueleka  mchezo wa kesho kila mmoja yuko vizuri na ana ari kubwa, jambo muhimu kwetu ni kushinda mchezo huo ili tumalize ligi kwa heshima, hatuna wasiwasi wowote tuko salama kwenye msimamo wa ligi, kumaliza kwa ushindi kutatuweka kwenye mapumziko mazuri  kwa matayarisho ya msimu mpya”, alisema.

Kuhusu  majeruhi Katepa  alisema kuwa City itakosa huduma ya nahodha na mlinzi shupavu wa kushoto Hassan Mwasapili alaiye majeruhi kufuatia maaumivu ya nyama za paja  yanayomkabili, pia  Temi Felix na Deo Julius  hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho kupisha majeraha waliyonayo.

“Mkuu wa kitengo  chetu cha utabibu Dr Joshua kaseko, amenieleza asubuhi kuwa  tutawakosa wachezaji hao kutokana na majereha waliyonayo hii ina maana kuwa wataonekana uwanjani  wakati wa matayarisho ya msimu mpya, mwalimu tayari kashafanya utaratibu wa wale wataochukua nafasi zao hivyo tuna uhakika wa kuingia uwanjani na kikosi kilicho bora licha ya kutokuwepo kwa nyota hao” alimaliza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here