Home Dauda TV VIDEO: MAPOKEZI YA YANGA, NYOMI LAKE NI HATARI

VIDEO: MAPOKEZI YA YANGA, NYOMI LAKE NI HATARI

732
0
SHARE

Mabingwa mara mbili mfululizo wa VPL klabu ya Yanga leo imeingia jijini Dar es Salaam ikitokea Angola ilikokwenda kucheza mchezo wa marudiano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika ambako licha ya kupoteza mchezo wao lakini wamefanikiwa kufuzu kwa hatua hiyo.

Umati mkubwa wa mashabiki umejitokeza kuipokea timu yao wakati inarejea Dar na kuujaza uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Intenational Airport.

Mashabiki ha hawakuishia uwanja wa ndege, waliongozana na basi lililobeba wachezaji kuelekea makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Twiga na Jangwani, Kariakoo.

Timu nzima ya shaffihdauda.co.tz ilikuwepo eneo la tukio na kufatilia kwa karibu mapokezi hayo ya aina yake na hapa inakuletea picha za matukio kadhaa za matukio mbalimbali yaliyojiri

Angalia video ushuhudie yote yaliyojiri uwanja wa ndege na barabari Yanga walivyoiteka Dar

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here