Home Kitaifa Kwa shabiki wa Man Utd mwenye wasiwasi na fainali ya kesho –...

Kwa shabiki wa Man Utd mwenye wasiwasi na fainali ya kesho – hizi ni rekodi za LvG kwenye fainali

569
0
SHARE

Kwa wale mashabiki wa Manchester United wanahofia matokeo mabaya kwenye mchezo wa wikiendi hii wa fainali ya FA Cup – wanaeza kupata ahueni kwa kuangalia rekodi ya Louis Van Gaal kwenye hatua ya fainali.

 United wanapewa nafasi kubwa ya kuifunga Crystal Palace – klabu ambayo haijawahi kushinda kombe lolote kubwa na hii ndio mara yao ya pili kucheza fainali ya FA Cup.

Japokuwa umekuwa msimu mgumu kwa mashetani wekundu – wakishindwa kumaliza kwenye top 4, jambo linalomaanisha watakuwa hawana hali ya kujiamini kuelekea mchezo dhidi ya Palace.

Lakini ukiangalia rekodi ya Van Gaal kwejye hatua ya fainali – unapata picha kwamba mashabiki wa United wanapaswa kuwa na matumaini ya kuondoka Wembley wakiwa washindi.

 Wakati akiwa kocha wa vilabu vya Ajax, Barcelona na Bayern Munich  – mdachi huyu ameshiriki kwenye fainali sita za makombe makubwa na amepoteza mara moja tu. Alishinda kombe la ligi la Uholanzi, Spain na Ujerumani pamoja na UEFA Cup na Champions League akiwa na Ajax. Mechi pekee ya fainali kwa Van Gaal kupoteza ilikuwa katika fainali ya  msimu wa 1995/96 ya Champions League na Ajax na 2009/10 akiwa na Bayern.

LVG ana wastani wa 83.3 wa kushinda fainali – miongoni mwa rekodi bora kwa makocha duniani. Jose Mourinho ambaye amecheza fainali 12 na Pep Guardiola ambaye ameziongoza timu zake kwenye fainali 6 – wote wana wastani sawa na LVG.

Kocha pekee ambaye anamzidi LVG kwa wastani mkubwa wa kushinda fainali ni Carlo Ancelotti ambaye ana wastani wa 85.7.

 Mpinzani wa LVG jumamosi ya kesho ni Alan Pardew ambaye amefanikiwa kucheza fainali akiwa kocha mara moja tu – akiwa kocha wa West Ham mwaka 2006. Alipoteza fainali hiyo mbele ya Liverpool iliyokuwa ikiongozwa dimbani na Steven Gerrard.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here