Home Dauda TV VIDEO: OZIL AIBUKA KAMBI YA WAKIMBIZI NA KUCHEZA MPIRA NA WATOTO

VIDEO: OZIL AIBUKA KAMBI YA WAKIMBIZI NA KUCHEZA MPIRA NA WATOTO

971
0
SHARE

Ozil-wakimbizi

Akiwa ameshamaliza msimu wa ligi na klabu yake ya Arsenal huku akijiandaa kwenda kuipeperusha bendera ya Ujerumani kwenye michuano ya Euro, star wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil ametumia muda wake kutembelea kambi ya wakimbizi na kucheza mpira na watoto.

Kiungo huyo mchezeshaji aliyeshinda kombe la dunia mwaka 2014 hivi karibuni ametembelea kambi ya wakimbizi huko Jordan na akaelezewa kwa ufupi hali ya maisha ya watoto ilivyokuwa ngumu katika kambi hiyo. Lakini watoto walifurahishwa na kitendo cha Star huyo, Ozil aligawa mipira ya soka, cap za baseball baada ya kucheza pamoja na watoto hao.

Mashabiki wa Arsenal huenda wakahuzunishwa kutokana na kitendo cha Ozil kuamua kusogeza mbele mazungumzo ya kuongeza mkata mpya na klabu hiyo hadi pale fainali za mataifa ya Ulaya zitakapomalizika nchini Ufaransa.

Kuhusiana na kuongeza mkataba mpya na The Gunners, Ozil amesema: “Bado nina miaka miwili kwenye mkataba wangu na Arsenal na kwasasa naweka akili yangu yote kwenye michuano ya Euro 2016, kitakachotokea kuhusu Arsenal tutaona baadaye sote kwa pamoja”.

Ozil amefanikiwa kupiga pasi nyingi za magoli kwa upande wa Arsenal msimu huu kwa kufanikiwa kutengeneza magoli 19 kwenye Premier League.

Angalia watoto walivyofurahi kukutana na nyota wa Arsenal na kucheza nae mpira kwenye kambi ya wakimbizi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here