Home Ligi EPL ADEBAYOR KAFANYA MAAMUZI MENGINE KUHUSU MAISHA YAKE YA SOKA

ADEBAYOR KAFANYA MAAMUZI MENGINE KUHUSU MAISHA YAKE YA SOKA

598
0
SHARE

3099B64200000578-3417775-Adebayor

Striker wa zamani wa Tottenham Hotspur Emmanuel Adebayor amesema ataachana na klabu ya Crystal Palace baada mchezo wa fainali ya FA Cup mwishoni mwa juma hili, taarifa hii ni kwa mujibu wa The Mirror.

Adebayor, 32, alisaini mkataba wa miezi sita kuitumikia klabu ya Palace, amethibitisha kwamba, ataondoka ndani ya Selhurst Park baada ya mchezo wa fainali ya FA Cup dhidi ya Manchester United utakaochezwa kwenye dimba la Wembley simu ya Jumamosi.

“Nilikuwa na miezi sita hapa. Natamani kama ningeendelea kucheza zaidi kwenye klabu hii lakini hii ndiyo soka. Safari itasimama May, lakini hiyo siyo mwisho wa safari yangu. Itasaimama tu. Itaendelea tena, popote pale ntakapokwenda. Siku zote nitaitakia mema klabu hii”, amesema mtogo huyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here