Home Kimataifa MAMBO 5 USIYOYAJUA KUHUSU DIEGO SIMEONE ‘EL CHOLO’

MAMBO 5 USIYOYAJUA KUHUSU DIEGO SIMEONE ‘EL CHOLO’

821
0
SHARE

Simeone

Diego Simeone ni kocha wa Atletico Madrid ambaye tarehe 28 Mei,atakiongoza kikosi chake kucheza fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Real Madrid. Mfahamu Diego Simeone kwa undani zaidi;

  1. FAMILIA YA MPIRA

Baba yake Carlos Alberto Simeone alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu wa ridhaa. Kaka yake na mdogo wake wanacheza River Plate. Vile vile Dada yao ni mmoja wa wakala wao.

  1. MAISHA YA SOKA

Diego Simeone alikuwa anacheza kama kiungo mkabaji na alianza maisha ya mpira katika timu ya Velez Sarsfield nchini Argentina kisha akaenda Sevilla, Inter Milan na Lazio ambako alipata mafanikio makubwa kwa kushinda makombe 4 ndani ya mwaka mmoja. Mwaka 1994 hadi 1997 aliitumikia Atletico Madrid kisha kurudi tena mwaka 2003 hadi 2005.

  1. AMKUTA TORRES NAHODHA

Fernando Torres ni mmoja wa wachezaji tegemezi wa kikosi cha Atletico Madrid kinachonolewa na Diego Simeone. Baada ya Simeone kurejea kwa mara ya pili Atletico Madrid alimkuta Torres ndiye nahodha wa timu hiyo baada ya kuwa mfungaji bora wa klabu kwa misimu miwili mfululizo. Simeone alikaa kwa miaka miwili na kuelekea zake kwao Argentina na Torres alienda zake Liverpool nchini Uingereza.

  1. AJIFUNGIA BAFUNI KWA NUSU SAA

Februari 16 mwaka 2006, Diego Simeone alicheza mechi yake ya mwisho kama mchezaji. Baada ya mechi kumalizika Simeone alijifungia bafuni kwa nusu saw akitafakari nini afanye baada ya kustaafu mpira. Ndipo alipoamua kuwa kocha.

  1. AFANANISHWA NA ‘THE SPECIAL ONE’

Makeke yake na mbinu zake zimemfanya afananishwe na kocha wa Kireno, Jose Mourinho. Hata kwa mafanikio kidogo kwa Simeone si haba sana alifanikiwa kushinda makombe 2 ndani ya miaka mitatu nchini Argentina. Mwaka wake wa kwanza kama kocha wa Atletico Madrid afanikiwa kushinda kombe la Europa league.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here