Home Ligi EPL Sababu 5 za kitakwakimu kwanini Van Gaal anahitaji kufukuzwa Man United

Sababu 5 za kitakwakimu kwanini Van Gaal anahitaji kufukuzwa Man United

512
0
SHARE

Anguko la MANCHESTER UNITED chini ya Louis van Gaal linadhihirika wazi na takwimu mbalimbali zinaonyesha madhaifu yao katika Premier League msimu huu.

image

Van Gaal yupo katika hatihati kufukuzwa kutoka Old Trafford baada ya kufeli kupata nafasi ya kucheza Champions League msimu ujao pamoja na kutumia £250million kufanya usajili.

Kocha huyo wa kidachi amekuwa akisisitiza kwamba kikosi kinacheza soka la kushambulia pamoja na kukosolewa kwa kucheza soka lilopooza na mashabiki wa klabu hiyo.
Na takwimu za msimu zinathibitisha bila mashaka Van Gaal ameifanya United kuwa imara nyuma na dhoofu mbele kwenye udhambuliaji.

image

Ni timu tatu pekee katika Premier League ambazo zina wastani mdogo wa kupiga mashuti langoni kuliko Manchester United, timu hizo ni Aston Villa iliyoshuka daraja pamoja na Newcastle na nyingine ni West Brom.

United wamepiga mashuti 418 langoni mwa wapinzani katika msimu mzima, namba sawa na Norwich, wamezidiwa kwa mara 241 ya mashuti waliyopiga Spurs ambao ndio wanaongoza.

Pamoja na kwamba United wamekuwa wakigombea nafasi nne za juu msimu mzima, lakini hawakuwa tishio kwa safu za ulinzi za wapinzani kama ilivyo kwa timu nyingine.

image

Wanashika nafasi 7 katika listi ya waliofunga magoli mengi kwenye ligi – wakiwa wamefunga magoli 46 – magoli mawili nyuma ya Sunderland ambao wameepuka kushuka daraja hivi karibuni.

image

Van Gaal amekuwa akitetea sana staili ya uchezaji wa timu yake lakini namba hazidanganyi – Manchester United ni moja ya timu zinazoongoza kwa kupiga pasi za kwenda pembeni kwenye Premier League – 3107, ni timu mbili tu ambazo zimepiga pasi za pembeni kuwazidi wao msimu mzima.

image

Ni muda sahihi umefika wa United kuachana na LVG – ni wazi mbinu zake zimefeli na zinaendana kinyume na soka halisi la utamaduni wa Manchester United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here