Home Dauda TV VIDEO: MTOTO WA CAZORLA ADHIHIRISHA MAJI HUFUATA MKONDO

VIDEO: MTOTO WA CAZORLA ADHIHIRISHA MAJI HUFUATA MKONDO

672
0
SHARE

Cazorla Jr

Baada ya mchezo wa jana kati ya Arsenal na Aston Villa ambapo Arsenal walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, wachezaji waliingia na familia zao uwanjani wakiwaaga mashabiki wao na kujiandaa na msimu mpya.

Kitu cha kuvutia ni pale mtoto wa kiungo ‘kisheti’ na mwenye ‘udambwidambwi’ wa Arsenal Santi Cazorla, Enzo Cazorla alipoonesha ufundi wa ajabu kwa kuwakimbiza watoto wa wachezaji wengine wa Arsenal kama vile Francis Coquelin.

Mtoto huyo ameonekana ni mwenye kipaji cha aina yake na ni kama vile anafuata nyayo za baba yake.

Angalia video mtoto wa Cazorla anavyozifuta nyayo za baba yake

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here