Home Kitaifa AZAM, SIMBA, MWADUI, MTIBWA ZILIVYOSHIKILIA ‘UHAI’ WA MGAMBO, RUVU, SPORTS, KAGERA VPL

AZAM, SIMBA, MWADUI, MTIBWA ZILIVYOSHIKILIA ‘UHAI’ WA MGAMBO, RUVU, SPORTS, KAGERA VPL

604
0
SHARE

Azam vs Ruvu 5

Baraka Mbolembole

Azam FC, Simba SC, Mtibwa Sugar na Mwadui FC zina uhakika wa kuendelea kucheza ligi kuu ya kandanda Tanzania Bara (VPL) msimu ujao, lakini upande mwingine klabu nne zinategemea ‘kubebwa’ na timu hizo ili ziendelea kufurahia VPL msimu wa 2016/17.

Ni rahisi Kagera, Sports kubaki VPL kuliko Azam, Simba kufungwa na Mgambo, JKT Ruvu.

African Sports ambayo ilipoteza 2-1 dhidi ya Azam FC siku ya jana Jumapili katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga na kushuka hadi nafasi ya 15 ya msimamo. Mabingwa hawa wa Tanzania 1988 walikuwa ligi za chini kwa miaka 23 kabla ya kurejea tena VPL msimu huu imekusanya pointi 26 katika michezo yao 29 na kitendo cha kushindwa kupata ushindi katika game ya mwisho katika uwanja wa Manungu Complex, Turiani dhidi ya Mtibwa Sugar mwishoni mwa wiki hii kitaashiria kushuka daraja kwa mara nyingine kwa timu hiyo.

Kuifunga Mtibwa pia huenda kusitoshe kuwabakisha Sports katika ligi kuu msimu ujao labda itokee JKT Ruvu, Kagera Sugar na JKT Mgambo zishindwe katika michezo yao ya mwisho. Tayari Coastal Union ya Tanga imeteremka daraja, na msimamo wa ligi baada ya kila timu kucheza game 29.

Coastal wamezibeba timu zote wakiwa na alama 22, Sports wanafuatia wakiwa na pointi 26, Mgambo ipo nafasi ya 14 (nafasi ya mwisho kwa timu 3 zinazopaswa kushuka daraja,) wamefikisha alama 27 kufuatia ushindi wao wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani siku ya Jumamosi iliyopia.

Kagera ambayo iliichapa Stand 2-1 siku ya jana Jumapili ipo nafasi ya 13 ikiwa na alama 28 na timu ya mwisho iliyo hatarini zaidi JKT Ruvu imekusanya alama 29 hadi sasa ikiwa nafasi ya 12. Timu hizi nne kila moja inaombea mwenzake ipoteze mechi na yenyewe ishinde. Sare ya 2-2 katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi dhidi ya Azam FC siku ya mwisho ya msimu uliopita iliwabakisha Mgambo VPL na msimu wao wa nne katika ligi kuu wanarejea tena katika uwanja ule ule ili kuepuka jaribio baya zaidi la kutoshuka.

Safari hii pointi moja haitawatosha hata kama Kagera watapoteza mchezo au kupata sare, labda itokee wapoteze mechi kwa idadi ya zaidi ya magoli matatu. Ni ushindi tu dhidi ya Azam ndiyo utawabakisha Mgambo VPL msimu ujao vinginevyo ‘wanakwenda na maji.’

Azam inahitaji ushindi pia ili wamalize katika nafasi ya pili kwa mara ya tatu ndani ya misimu minne ambayo wameshinda taji moja. Wakiwa na alama 63, Azam wanaweza kupitwa na Simba ikiwa watashindwa kuifunga Mgambo na ‘Wekundu wa Msimbazi’ kuishinda JKT Ruvu.

Mtibwa imeshushwa hadi nafasi ya tano baada ya kuchapwa 1-0 na Simba katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro siku ya jana na Tanzania Prisons wamepanda hadi nafasi ya nne kufuatia ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Sokoine, Mbeya na kuwafanya ‘ wajela jela’ wafikishe alama 48-pointi moja zaidi ya Mtibwa.

Sports wanaweza kuepuka ‘kimaajabu’ kutoshuka kama wataifunga Mtibwa na kuomba Mgambo na JKT Ruvu zipoteze mechi zao. Wakati sare tu dhidi ya Simba itawabakisha ligi kuu JKT Ruvu, ikiwa Ruvu itakubali kufungwa  halafu Sports ikishinda itawafanya walingane pointi kwa maana hiyo uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa utaamua nani mbabe kati yao (Ruvu-wana wastani wa hasi 42 na Spots wana wastani wa hasi 31 wa magoli ya kufunga na kufungwa.)

Kwa maana hiyo unaweza kuona timu itakayokuwa juu ya mwenzake ikitokea wakafungana  kwa pointi. Kagera itakuwa na nafuu kiasi, kwa kutumia uzoefu wa kuwafunga Stand ‘wembe’ wao huo unaweza kuwabikisha VPL kama watautumia vivyo hivyo dhidi ya Mwadui FC mwishoni mwa wiki hii. Ushindi wa aina yoyote utakuwa umewanusuru kimaajabu kutoshuka.

Timu zenye uwezekano mkubwa wa kushuka ni JKT Ruvu na JKT Mgambo na zilizo na uwezekano mkubwa kubaki ni Sports na Kagera kulingana na michezo ya kufunga msimu itakavyokuwa wikendi ijayo.

Mgambo kuifunga Azam itamaanisha ni timu ya pili kufanya hivyo dhidi ya Azam katika uwanja wa Chamanzi. JKT Ruvu kuishinda Simba uwanja wa Taifa itamaanisha ‘kukivunja’ kabisa kikosi cha ‘Wekundu wa Msimbazi’, Kagera kuishinda Mwadui ni jambo rahisi baada ya kuwa katika nyakati ngumu kwa msimu mzima, Sport itakuwa timu pekee ya Tanga kusalia VPL ikiwa itaifunga Mtibwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here