Home Kitaifa YANGA KUKABIDHIWA TAJI LA 26 NA WAZIRI NCHEMBA

YANGA KUKABIDHIWA TAJI LA 26 NA WAZIRI NCHEMBA

577
0
SHARE

Mwigulu Nchemba

Na Baraka Mbolembole

Ofisa habari wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, Alfred Lucas amethibitisha kwamba Waziri wa Kilimo na Mifugo, Mh. Mwigulu Nchemba ndiye atakayekuwa mgeni rasmi katika pambano la ligi kuu Tanzania Bara kati ya wenyeji Ndanda SC dhidi ya mabingwa Yanga SC siku ya leo (Jumamosi) katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pambano hilo ambalo litatumika kuwakabidhi kombe la ligi hiyo timu ya Yanga awali lilikuwa lifanyike katika uwanja wa Nangwanda, Mtwara ambao ni uwanja wa nyumbani wa Ndanda lakini Yanga wakaomba kwa wapinzani wao hao mechi hiyo ifanyike katika uwanja wa Taifa kwa sababu watasafiri siku ya Jumapili kuelekea Angola ambako watacheza na Esperanca ya huko katikati ya wiki ijayo katika game ya marejeano ya michuano ya Shirikisho Afrika.

“Bodi ya ligi pamoja na Shirikisho la soka nchini wamekubaliana Mheshimiwa, Mwigulu Nchemba ambaye ni Waziri wa Kilimo na Mifugo ndiye atakayekuwa mgeni rasmi katika mtanange wa ligi kuu kati ya wenyeji Ndanda dhidi Yanga katika uwanja wa Taifa anasema Lucas na kufafanua zaidi kwa nini mchezo huo utachezwa uwanja wa Taifa badala ya Nang’wanda.

“Pengine nieleze kitu moja, Ndanda wametumia kanuni ya pili ya ligi kuu Tanzania Bara toleo la 2015 kucheza mchezo huu katika uwanja wa Taifa hasa ukizingatia maombi ya Yanga ambayo yalikubaliwa na Ndanda. Yanga watasafiri siku ya Jumapili kwenda Angola hivyo waliomba mechi ifanyike Dar es Saalam ili kupunguza uchovu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here