Home Ligi EPL Kitakachotokea kwenye kufuzu Europa – ikiwa Liverpool watafungwa fainali ya Europa na...

Kitakachotokea kwenye kufuzu Europa – ikiwa Liverpool watafungwa fainali ya Europa na Sevilla 

683
0
SHARE

West Ham na  Liverpool wanaweza kujikuta wanapambana kwenye mchezo wa play off wa kugombea kufuzu kucheza Europa League.

image

Wagonga nyundo wa London wanashika nafasi ya sita katika Premier League kabla ya mchezo wa mwisho, wakati Liverpoool wanashika nafasi ya 8.

Liverpool wanacheza na Sevilla kwenye fainali ya Europa League huku wakijua kwamba ushindi utawafanya wapate Nafasi ya kushiriki michuano ya mabingwa wa ulaya.

Ikiwa itawabidi kufuzu Europe kupitia ligi, kuna uwezekano Reds na West Ham huenda wakamaliza sawa kwa pointi, uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa.

PLAY OFF Itafanyika nini kikitokea?

image

Ikitokea West Ham wakafungwa 1-0 na Stoke City na Liverpool wakaifunga West Brom 2-1 au Wagonga Nyundo wakafungwa 2-1 na Liverpool ashinde 2-1 na kwa bahati mbaya wanaoshika nafasi ya 7 Southampton wasipate matokeo ya ushindi dhidi ya Crystal Palace. Matokeo haya yatawaacha Hammers na Liver wakifanana kinamba kwenye ligi baada ya kucheza zote 38.

Na haya niliyoeleza hapo juu yakitokea basi itabidi ufanyike mchezo wa mtoano wa kuamua yupi atakayefuzu kucheza Europa msimu ujao. Ila haya yote pia yatategemea na Sevilla kushinda mechi ya wiki ijayo dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp.

Msemaji wa Premier League amethibitisha mchezo wa ziada itabidi ufanyike ikitokea matokeo ya namna hiyo yametokea – jambo lina nafasi ndogo kutokea.

Namna ya kufuzu Europa League

image

Manchester City tayari wamejihakikishia angalau kucheza Europa League msimu ujao baada ya kushinda Capital One Cup.

Ikiwa watamaliza katika Top 4 , nafasi hiyo ya kucheza raundi ya 3 ya kufuzu Europa League itaenda kwa mshindi wa 6 kwenye ligi.

Jambo kama hilo linaweza kutokea ikiwa watafuzu kucheza Europa League hatua ya makundi ikiwa watamaliza nafasi ya 5 kwenye ligi.

Ikiwa Liverpool watashinda Europa League,  watafuzu kucheza Champions League hatua ya makundi. Ikiwa Crystal Palace watashinda FA Cup, wataingia hatua ya makundi kwenye Europa League, na ikiwa Manchester United watashinda, basi nafasi hiyo watapewa walioshika nafasi ya 7 kwenye ligi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here