Home Kitaifa MGOSI: WACHEZAJI WA SIMBA TUNASTAHILI KUUAWA

MGOSI: WACHEZAJI WA SIMBA TUNASTAHILI KUUAWA

1047
0
SHARE
Mshambuliji na nahodha wa kikosi cha Simba SC Mussa Hassan Mgosi
Mshambuliji na nahodha wa kikosi cha Simba SC Mussa Hassan Mgosi
Mshambuliji na nahodha wa kikosi cha Simba SC Mussa Hassan Mgosi

Mshambuliaji mkongwe na nahodha wa kikosi cha Simba SC Musa Hassan ‘Mgosi’ ameshindwa kujizuia kuonesha kusikitishwa na matokeo mabaya ya klabu yake katika siku za hivi karibuni na kufikia kusema wachezaji wote wa Simba ndiyo wanastahili kubeba lawama za matokeo hayo na si mtu mwingine yeyote.

Mgosi hakuishia hapo akaenda mbali zaidi na kusema anadhani wachezaji wa Simba wanastahili kuuawa wote kwasababu hawaitendei haki timu yao.

Inasikittisha sana, kwa mtu mwenye akili timamu na anayejua Simba inataka nini, lazima aumie. Nafikiri kama ingekuwa kwenye nchi nyingine basi ningeruhusu wachezaji wote tuuawe kwasababu hatuitendei haki Simba.

“Kila siku tumekuwa tukisema wenzetu wanapendelewa, sisi tunapata nafasi tunashindwa kuzitumia mwisho wa siku lazima lawama tukubali sisi. Mechi ambazo ni muhimu kwetu tunashindwa kucheza, hakuna kulaumu kiongozi, kocha wala mtu mwingine yeyote, kwasababu wao wanatimiza majukumu yao wanapeleka timu kambini, watu wanakula, mishahara wanapata, tukishinda bonus inatolewa sasa hapo kiongozi analaumiwa vipi?”, anahoji Mgosi ambaye alipata mafaniko na simba katika miaka ya 2005 hadi 2011.

“Lawama zote tupokee sisi wachezaji ndiyo tunasababisha Simba iwe hivi”, alimaliza nyota huyo aliyetamba na Mtibwa katika misimu ya 2013-14 na 2014-15 kabla ya kurejea tena Msimbazi msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here