Home Kimataifa Kutoka Lisbon mpaka Milan: Mabadiliko yaliyotokea kwa Atletico Madrid na Real Madrid

Kutoka Lisbon mpaka Milan: Mabadiliko yaliyotokea kwa Atletico Madrid na Real Madrid

1245
0
SHARE

Real Madrid na Atletico madrid kwa mara nyingine tena watakutana katika mchezo wa kuamua yupo ni bora barani ulaya, hata hivyo mengi yamebadilika tangu mara ya mwisho timu hizi zilipokutqna katika fainali ya ulaya. 

14624445857668

Miaka miwili na nusu tangu walipokutana Lisbon, timu mbili za Madrid wanategemewa kuwa na mabadilijo ya wachezaji watano au sita katika kila kikosi kwenye fainali ya jijini Milan. Real Madrid wana mabadiliko makubwa zaidi kuanzia kwenye benchi. Zinedine Zidane alikuwepo wakati wa fainali ya Lisbon lakini wakati huo alikuwa msaidizi wa Carlo Ancelotti lakini hivi sasa mfaransa huyo ndio kocha mkuu na anajua namna ya kushinda fainali – uzoefu ambao unaweza kuwa muhimu  katika mchezo wenye ukubwa wa aina hii. 

  Gwiji aa Madrid golikipa Iker Casillas hatimaye aliondoka baada ya kushinda ‘La Decima’ na mbadala wake akawa golikipa wa Costa Rica Keylor Navas ambaye amekuwa na msimu mzuri katika lango la Madrid. Kwenye safu ya ulinzi kuna mabadiliko mawili. Marcelo ataanza upande wa kushoto badala ya Fabio Coentrao ambaye alicheza kwenye nafasi hiyo miaka miwili iliyopita. Marcelo aliingia baada ya majeruhi na kwa hakika yeye alichangia kurudi kwa Madrid mchezoni na kubadili matokeo.

Katika fainali hiyo Pepe aliingia akitokea benchi  badala ya Raphael Varane. Hivi sasa hali imebadilika baada ya Pepe kurejea katika kiwango chake. 

Kwenye safu ya kiungo ndipo kwenye mabadiliko makubwa kwa upande wa Los Blancos – na ni Luka Modric pekee aliyebaki kwenye nafasi hiyo. Sami Khedira na Angel Di Maria wameshaondoka kwenye klabu. Badala yake Toni Kroos na Casemiro ambao wanategemewa kuanza mchezo huo wa fainali jijini Milan. 

  Washambuliaji wa mbele bado wapo vile vile, kama wasipopata majeruhi, Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Gareth Bale, wataanza mechi hii kama ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.

  Mabadiliko upande wa Atletico Madrid yalikuwa makubwa, iliwabidi wajivue gamba wazaliwe upya baada ya karibu nusu ya mastaa wao kuondoka baada ya fainali ya miaka miwili iliyopita. Imefanyika kazi nzuri sana na mkufunzi Diego Simeone ambaye atakuwa kwenye benchi kuiongoza timu yake kwenye fainali, May 28 huku nusu ya kikosi chake kikiwa kimebadilika. 

Jan Oblak kwa hakika ameziba pengo liloachwa wazi na Thibaut Courtois na hat kumzidi kitakwimu. Safu ya ulinzi ya Simeone ipo vizuri – mabadiliko pekee ni kuondoka kwa Miranda, hivyo Godin atacheza na Jose Maria Gimenez. Ni Gabi na Koke pekee ambao wamebaki kwenye safu ya kiungo. Wachezaji hawa wamekuwa uti wa mgongo wa timu na walipocheza fainali ya Lisbon waliungana na Tiago na Raul Garcia. Hata hivyo Tiago huenda akarejea kikosini baada ya kutoka kwenye majeruhi – Garcia aliondoka na huenda Saul na Agusto wakaziba mapengo yao

Safu ya ushambuliaji kila kitu kimebadilika – David Villa na Diego Costa wameondoka siku nyingi na kumuacha Antoine Griezmann na Torres wakiliongoza jahazi la Simeone.  

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here