Home Ligi EPL UBINGWA WA LEICESTER ILIKUWA NI HABARI MBAYA KWA STAR WA MISRI

UBINGWA WA LEICESTER ILIKUWA NI HABARI MBAYA KWA STAR WA MISRI

543
0
SHARE

Mido

Habari za Leicester kutwaa ndoo ya EPL zilikuwa mbaya kwa Mido ambaye ni mchezaji wa zamani wa  Tottenham.

Mido ambaye jina lake halisi ni Ahmed Hossam, alikuwa mchezaji wa Tottenham kuanzia mwaka 2005 hadi 2007 lakini hakupata mafanikio akiwa White Hart Lane.

Akiwa amewahi kuvichezea vilabu vya Ajax, Marseille, Roma, Middlesbrough pamoja na West Ham, ni mchezaza soka aliyewahi kujizolea umaarufu mkubwa Misri lakini kwa sasa anafanya uchambuzi wa masula ya soka katika kituo cha television cha beIN Sports.

Wakati wa msimu huu, kipindi Leicester imeshika kasi katika mbio za kuwania ubingwa wa EPL, Mido aliweka ahadi kwamba, endapo Leicester watatwaa ubingwa huo yeye atanyoa nywele zake zote na kubaki kipara.

Nywele za Mido ni muhimu kwake kutokana na kumtambulisha, lakini alizinyoa siku ya Jumamosi kutimiza ahadi yake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here