Home Kitaifa KOCHA WA ESPARANCA AIWASHIA YANGA TAA YA KIJANI MAKUNDI CAF

KOCHA WA ESPARANCA AIWASHIA YANGA TAA YA KIJANI MAKUNDI CAF

568
0
SHARE
Kocha mkuu wa Esparanca Zoram Manojlovec (kulia) amesema timu yake inanafasi ndogo ya kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho ukilinganisha na Yanga
Kocha mkuu wa Esparanca Zoram Manojlovec (kulia) amesema timu yake inanafasi ndogo ya kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho ukilinganisha na Yanga
Kocha mkuu wa Esparanca Zoram Manojlovec (kulia) amesema timu yake inanafasi ndogo ya kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho ukilinganisha na Yanga

Kocha wa GD Sagrada Esperanca Zoram Manojlovec anasema kipigo cha magoli 2-0 walichokubali kutoka kwa Yanga kinawapa nafasi finyu ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo kwasababu kubadili matokeo wakiwa Angalo itakuwa ni vigumu kwasababu Yanga watahitaji sare yeyote tu ambayo itawafanya wafuzu kwenda kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

“Kipindi cha pili Yanga walicheza vizuri sana na wakapata goli, matokeo yangebaki 1-0 angalau tungeendelea kujipa moyo kwenye mechi ya marudiano, lakini goli la pili limetumaliza. Tutacheza nyumbani mchezo wa marudiano laiki matokeo ya kupoteza kwa goli 2-0 ni magumu kwetu.”

“Tuna dakika nyingine 90, inawezekana tukafanya jambo jambo ni vigumu sana kwa upande wa timu yangu. Tulipotea kuanzia dakia ya 70, Yanga wakapata nafasi ya kutufunga goli la pili kwa shuti la mbali, lakini ndiyo mpira.”

“Ni ngumu kubalisha matokeo haya lakini inawezekana. Mfano mzuri ni fainali ya Champions League kati ya Liverpool dhidi ya AC Milan walianza kwa kupoteza kipindi cha kwanza kwa magoli matatu lakini Liverpool wakasawazisha na kushinda kombe.”

Yanga ikiitoa Esparanca katika hatua hii, itakuwa imefuzu kwenda hatua ya nane bora (hatua ya makundi) ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu za Tanzania kufanya hivyo tangu Simba walipofuzu katika hatua hiyo katika mashindano ya kbabu bingwa Africa mwaka 2003.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here