Home Kitaifa WACHEZAJI 6 WALIOTEMWA SIMBA, WANATAMBA MBELE YA SAFARI

WACHEZAJI 6 WALIOTEMWA SIMBA, WANATAMBA MBELE YA SAFARI

10255
0
SHARE

Hassan-Kessy Ramadhani

Katika miaka ya hivi karibuni Simba kufanya vizuri katika ligi ya Bongo na kupelekea kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya CAF ambayo imetawaliwa na Yanga na Azam. Ukitaka kujiuliza kwa nini Simba imeshindwa kufanya vizuri utagudua ni pamoja na kuwaacha wachezaji wakemuhimu  ambao wangeisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano ya ndani pengine na ile ya kimataifa.

Wachezaji wamekuwa wakiihama klabu hiyo kwa figisufigisu nyingi sana, hebu jiulize mara ya mwisho Simba kumuuza mchezaji kwenda klabu nyingine ilikuwa lini? Badala yake wachezaji wamekuwa wakiihama kwa migogoro au kwa kumalizika kwa mikataba na kuondoka bure bila Simba kupata hata jero tu!

Anza na enzi za Kelvin Yondani, Athumani Idd ‘Chuji’, njoo hapa kwa Haruna Chanongo, Simba wanabaki kujivunia kuwauza Mbwana Samatta na Emanuel Okwi. Lakini siku za hivi kariuni klabu hiyo imekua ikiwatema au kukimbiwa na wachezaji ambao wameenda kutamba kwenye vilabu vingine baada ya kuonekana si kitu pale Msimbazi.

Kutana na orodha ya nyota wa Simba ambao walionekana ‘si lolote si chochote’ ndani ya Msimbazi lakini kwa sasa ni lulu huko waliko halafu vuta picha kama wangekuwepo Simba leo ingekuwa wapi?

Christopher  Edward-Toto Africans

Edward Christopher

Mshambuliaji huyu kijana ni miongoni mwa vijana wengi waliotemwa Simba kwa mizengwe na kuchukuliwa na kocha wa Toto African John Tegete kisha kuaminiwa na kupewa nafasi kwenye kikosi hicho cha Rock City. Kwa sasa ni miongoni mwa nguzo muhimu ambazo Toto inajivunia kuwa nao kwenye kikosi chao.

Kwenye mchezo wa marudiano wa VPL pale uwanja wa taifa, Edward alikuwa ni mwiba kwa safu ya ulinzi ya Simba na kupelekea beki wa pembeni Hassan Kessy kulambwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya mshambulizi huyu wa zamani wa kikosi hicho cha msimbazi.

Ikumbukwe kwenye kikosi cha Toto kilichoanza mchezo huo dhidi ya Simba kulikuwa na wachezaji takribani watano (Carlos, Chuku, Hassan Hatib, Edward Christopher, Japhet (sub) ambao walitemwa na Simba na wakaisaidia Toto kuichapa Simba bao 1-0 na kutibua mbio zao za ubingwa wa ligi msimu huu.

Ibrahim Twaha ‘Messi’-Coastal Union

Ibrahim Twaha

Kinda mwingine ambaye alianzia maisha yake ya soka katika kikosi cha vijana cha Simba na kunesha uwezo mkubwa kiasi cha kuwafanya wengi kuweka matumaini makubwa kwake kuwa ni miongoni mwa nyota watakaotamba siku za badae na kuweka klabu hiyo ya Msimbazi katika utawala wa soka la Tanzania.

Lakini tofauti na matarajio ya wengi, Twaha hakudumu Msimbazi na kutimkia Coastal Union ambako baada ya muda alirejeshwa tena Msimbazi kabla ya kutimkia tena kwenye klabu hiyo ya Tanga ambako yupo hadi sasa kwenye kikosi ambacho tayari kimekuwa cha kwanza kuiga ligi kuu ya Vodacom msimu huu.

Ibrahim Twaha ni kijana mwenye uwezo mkubwa lakini Simba walikosa uvumilivu wa kuendelea kumtunza kijana huyu ambaye amekuwa pamoja na vijana wengine kama Ajib, Ndemla, Hassan Isihaka, Mkude na wengine wengi.

Elias Maguri-Stand United

Maguri

Mshambuliaji huyu wa zamani wa Tanzania Prisons na Ruvu Shooting, alitemwa kwenye kikosi cha Simba bila kuambiwa sababu ya msingi na uongozi wake. Akiwa amesajiliwa kutoka Ruvu shooting baada ya kuonesha uwezo wa hali ya juu katika kupasia kamba, hakuwa na maisha marefu ndani ya Msimbazi baada ya kutemwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa msimu huu wa ligi.

Akiwa amefunga magoli manne kwenye mechi za kirafiki visiwani Zanzibar alitupwa nje ya kikosi hicho mara baada ya kurejea jijini Dar. Baada ya uongozi wa klabu hiyo kutaja majina ya wachezaji wanaongia kambini kujiandaa na mchezo wa Simba Day jina la mshambuliaji huyo halikuwepo miongoni mwa majina yaliyotajwa kuingia kambini na huo ndiyo ukawa mwisho wa maisha yake kwenye klabu ya Simba.

Stand United wakamnyakua Maguri ambaye alianza kwa kasi ya kufunga mfululizo na kupelekea kuitwa kwenye kikosi cha Stars na kocha Charles Boniface Mkwasa kujiandaa na mechi dhidi ya Nigeria ambapo alifunga goli kwenye mchezo dhidi ya Algeria uliomalizika kwa sare ya 2-2 kwenye uwanja wa taifa.

Amis Tambwe-Yanga SC

tambwe simba leo

Mshambuliaji huyu wa Yanga alitemwa na Simba kwa madai ameshuka kiwango, wakati huo akiwa ndiye anatetea kiatu chake cha ufungaji bora kwenye ligi. Baada ya kutemwa tu, Yanga wakamdaka na kumpa deal kwenye klabu yao ya kijani na manjano.

Tambwe akadhihirisha ubora wake katika msimu wake wa kwanza Yanga kwa maliza nyuma ya Msuva katika utupiaji kambani, Tambwe alifunga magoli 15 magoli mawili nyuma ya Msuva aliyenyakua tuzo ya mfungaji bora akiwa na magoli 17.

Mrundi huyo amezidi kuwa mwiba kwa timu yake ya zamani baada ya kuifunga kwenye mechi mbili za ligi walizokutana msimu huu. Kwa sasa Tambwe anamagoli 20 kwenye ligi akifuatiwa na Kiiza wa Simba mwenye magoli 19.

Simba bado mnamashaka na uwezo wa Tambwe? Kwasababu tayari ameshawanyoa mara mbili na sasa ndiye anaendesha gari la wanaowania kiatu cha ufungaji bora msimu huu.

Ramadhani Singano ‘Messi’-Azam FC

singano2

Kijana huyu mwenye upole mithili ya kobe aliyejiinamia akitunga sheria aliingia kwenye mgogoro mkubwa ulikuwa gumzo na kuibua mambo mengi yaliyokuwa yamefichika nyuma ya pazia. Simba walitaka kumuingiza ‘kingi’ Messi ambaye wamemlea na kumkuza wenyewe baada ya ‘kufoji’ mkataba wa Messi jambo ambalo alilistukia na kulipinga vikali.

Chama cha kutetea haki za wachezaji SPUTANZA nacho kikapambana kuhakikisha Messi anapata haki yake, mwisho wa siku mkataba huo ukapigwa chini na TFF na Messi akaachwa kama mchezaji huru kisha siku chache akajiunga kwenye kikosi cha Azam FC.

Messi ameshaanza kufanya vizuri ndani ya Azam huku akipata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara na ameisaidia klabu hiyo kupata ushindi katika mechi zake za ligi msimu huu pamoja na zile za kimataifa kabla ya kutolewa kwenye hatua ya 16 bora.

Hassan Kessy (-)

Ramadhani Kessy-Beki wa Simba SC
Ramadhani Kessy-Beki wa Simba SC

Kijana mwingine ambaye lilikuwa tumaini jipya katika nafasi ya ulinzi wa pembembeni ya klabu ya Simba, akiwa bado na umri mdogo tayari nyota huyu wa zamani wa Mtibwa Sugar ameshindwa kudumu Msimbazi na kuamua kuachana na klabu hiyo kwa njia ambazo si nzuri kutokana na uongozi wa klabu hiyo kushindwa kakaa na mchezaji huyo kutatua kasoro kadhaa baina ya pande hizo mbili.

Simba wanajifanya ‘maskini jeuri’ na hapo ndipo wanaumia, Kessy ameshawahi kugoma kuitumikia klabu hiyo mara kadhaa kutokana na kutotimiziwa baadhi ya vipengele vya mkataba wake. Kunawakati alikuwa anaidai klabu hiyo pesa za uhamisho wake pamoja na pesa la makazi kitu kilichopelekea waingie kwenye mgogoro kutokana na viongozi kutaka kumkandamiza aendelee kuchaza bila kupewa stahiki zake.

Siku za hivi karibuni uongozi umemfungia mchezji huyo kutokana na madai ya kupewa kadi nyekundu kwa makusudi na kughalimu timu yake kwenye kichapo cha bao 1-0 mbele ya Toto Africans. Mkataba wa Kessy na Simba unaisha mwishoni mwa msimu huu natayari kuna kila kitu kimeshakamilika mchezaji huyo anatua pale mitaa ya Twiga na Jangwani na msimu uja atakuwa akivalia jezi za Kijani na Njano.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here