Home Dauda TV VIDEO: ATLETICO YAITOA NISHAI BAYERN MUNICH

VIDEO: ATLETICO YAITOA NISHAI BAYERN MUNICH

684
0
SHARE

Atletico-Bayern

Atletico Madrid wametinga fainali ya Champions League kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu kwa kuitupa nje Bayern Munich kwa goli la ugenini kwenye mchezo wa marudiano wa nusu fainali.

Wakiwa na hazina ya ushindi wa goli 1-0 kutoka kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Hispania, Bayern wakasawazisha goli hilo kupitia free-kick ya Xabi Alonso iliyomgonga beki wa Atletico na kuzama wavuni.

Atletico-Bayern 1

Golikipa wa Atletico Jan Oblak alipangua penati ya Thomas Muller kabla ya Antoine Griezmann hajaisawazishia timu yake.

Robert Lewandowski aliipatia Bayern bao la pili kwa kichwa lakini Atletico walipambana baada ya Torres kupoteza mkwaju wa penati.

Atletico-Bayern 2

Bayern wakishangiliwa na kundi kubwa la mashabiki wao wa nyumbani walitakiwa kupata ushindi wa magoli 3-1 ili kujihakikishia nafasi ya fainali lakini hali ilikuwa ngumu kwao.

Ubora wa Oblak uliikosesha bao Bayern dakika za majeruhi pale alipozuia shuti kali la David Alaba akiwa umbali wa mita 20.

Atletico-Bayern 4

Atletico ambao wanatarajia kulitwaa taji la Ulaya kwa mara ya kwanza watakabiliana na Manchester City au Real Madrid kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa Milan May 28.

City watavaana Real Madrid ambao ni majirani za Atletico kesho Jumatano baada ya timu hizo kutoka sare kwenye mchezo wa kwanza juma lililopita.

Atletico kupoteza fainali ya tatu?

Atletico imepoteza michezo miwili ya fainali ya michuano ya Ulaya dhidi ya Bayern mwaka 1974 wakati huo kombe hilo likiitwa European Cup na dhidi ya wapinzani wao wa jadi Real Madrid miaka miwili iliyopita.

Wakicheza dhidi ya timu ambayo ilikuwa inacheza nusu fainali yake ya tano mfululizo, Atletico ilipambana hadi dakika zote 90 zinamalizika ndani ya Allianz Arena na kujizolea sifa katika idara yao ya ulinzi.

Mabingwa hao wa Ujerumani walifanya attempts 33 golini kwa Atletico na kufanikiwa kumiliki mpira kwa 72% lakini ilikuwa vigumu kupata walichokihitaji kutoka kwa wahispania.

The hallmark of Atletico’s recent success has been their strength in defence, with Diego Simeone’s side developing a reputation as one of the toughest teams in Europe to break down.

Atletico hawakufanya shambulizi hata moja ndani ya eneo la penati la Bayern kabla ya goli la Griezmann alilofunga akiwa nje kidogo ya box.

Pep Guardiola kachemka Bayern Munich

Atetico-Bayern 3

Pep Guardiola anaheshimika kwa kuwa ni miongoni mwa makocha bora duniani walioshinda mataji mengi akiwa na Barcelona na Bayern Munich.

Lakini mhispania huyu ataondoka kuelekea Manchester City akiwa amefeli kuwapa The Bavarians taji la Champions League ndani ya maiaka yake mitatu kwenye kikosi hicho.

Kikosi chake kimeshindwa kufurukuta dhidi ya timu za Hispania mara mbili kwenye hatua ya nusu fainali ndani ya misimu miwili iliyopita, ilichapwa na Real Madrid mwaka 2014 kabla ya kutandikwa na timu yake ya zamani FC Barcelona mwaka uliopita.

Licha ya kushinda mchezo wao wa 12 mfululizo wa Champions League kwenye uwanja wao wa nyumbani, lakini ushindi huo haukuwa na maana kwao.

Muller imekuwaje?

Muller alianzishwa kwenye kikosi cha kwanza cha Bayern Munich baada ya kuanzia benchi kwenye mchezo wa kwanza wili iliyopita jijini Madrid.

Guardiola alikosolewa na vyombo vya habari vya Ujerumani kwa uwamuzi huo wa kumuweka Muller nje akiwa amefunga magoli 32 kwenye michezo 46 msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa Ujerumani alishindwa kukwamisha kambani penati muhimu ambayo ilikuwa inaamua matokeo ya mchezo ambayo kama angefunga angeifanya timu yake iwe mbele mapema.

“Kukosa kwao penati, kulitupa uhai”, alisema kocha wa Atletico Madrd mara baada ya mechi.

Takwimu muhimu kuzifahamu

  • Atletico Madrid wamefuzu hatua ya fainali baada ya mchezo wao wa 100 kwenye michuano hiyo mikubwa Ulaya kwa ngazi ya vilabu.
  • Antoine Griezmann ni mfungaji anayeongoza kwa magoli mengi ndani ya historia ya Atletico Madrid kwenye  mashindano ya Champions League akiwa amefunga magoli tisa.
  • Katika penati mbili zilizopita kwenye michuano ya Champions League, Thomas Muller amekosa mara zote huku akiwa amefanikiwa kufunga mikwaju 7 kati ya 10 kwenye mashindano hayo.
  • Golikipwa wa Atletico Madrid Jan Oblak ameokoa penati ya pili kati ya tatu alizokutana nazo kwenye mashindano yote.
  • Magoli yote sita ya Xabi Alonso akiwa na Bayern ameyafunga akiwa nje ya box.
  • Goli la kwanza lililofungwa na Alonso ni mara ya kwanza kwa Atletico kuruhusu bao ndani ya dakika 632 kwenye mashindano yote.
  • Pep Guardiola ametupwa nje ya mashindano mara ya nne katika hatua ya nusu fainali ya Champions League.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here