Home Kitaifa MWINYI HAJI AMEAMUA KUFUNGUA KESI MAHAKAMANI KUPIGANIA JINA LAKE

MWINYI HAJI AMEAMUA KUFUNGUA KESI MAHAKAMANI KUPIGANIA JINA LAKE

2965
0
SHARE

Haji Mwinyi

Na Abubakar Kisandu, Zanzibar

Baba mzazi wa Mwinyi Haji Ngwali, mlinzi wa kushoto wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) amepania kulifungulia kesi gazeti la michezo la Bingwa baada ya kuandika habariinayomtaja motto wake kutumia madawa ya kulevya.

Gazeti hilo liliandika taarifa hiyo ndefu siku ya Jumamosi April 30 ambapo kichwa cha habari kilikuwa kimeandikwa “ SIRI NZITO YAFICHUKA YANGA”.

1 gazeti

Taarifa hiyo ambayo imeandikwa na mwandishi Hussein Omar, baba wa mchezaji huyo amesema msimamo wao ni kwenda mahakamani kulifungulia kesi gazeti hilo ili waandishi wa habari wapate funzo wanapoandika habari ziwe za uhakika na usahihi.

3 gazeti

“Nikiwa baba mzazi wa Mwinyi Haji Ngwali nasikitishwa kwa kitendo walichofanya gazeti la Bingwa la tarehe 30/04/2016 kwa kuandika kuwa mtoto wangu ni teja la kutupwa, hivyo kwa kitendo hicho wamelichafua jina la mtoto wangu na familia yetu, kwa hiyo tumeamua kama familia msimamo wetu ni kufungua madai mahakamani kwasababu baadhi ya waandishi wa habari wanakuwa hawapo sahihi kuandika habari zao” anasema mzee Haji.

2 gazeti

4 gazeti

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here