Home Kitaifa KOCHA VPL APATA ULAJI KENYA

KOCHA VPL APATA ULAJI KENYA

643
0
SHARE

Ramadhani Aluko

Aliyekuwa kocha mkuu wa African Sports Ramadhani Aluko amepata nafasi ya kwenda nchini Kenya kwenda kuinoa timu ya Kisumu Hot Star, inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini humo.

Aluko ambaye alivunjiwa kandarasi yake na African Sports kwa kile kinachodaiwa kuwa hakuweza kuiletea tija klabu hiyo, amekiri kuwa anakwenda nchini Kenya kukamilisha baadhi ya taratibu za mwisho za kuweza kufanya kazi nchini humo.

Pia amesema ameamuwa kufungua njia kwa Watanzania wengine kwenda kufanya kazi nje ya nchi na kuondokana na uoga  wa kutoka nje, pia amesema ni vizuri  kama kocha kuwa na jopo lako hivyo kama mambo yakienda vyema atachukuwa baadhi ya Waanzania akafanye nao kazi.

“Taarifa za mimi kwenda Kenya ni za kweli, kuna timu moja ambayo iko chini ya Gavana wa Kisumu amenipigia simu ananihitaji nikawe kocha mkuu wa timu yake inayoitwa Kisumu Hot Star na hadi muda huu tayari ameshatuma nauli, mambo mengine kimkataba naenda kuwasikiliza kama tukikubaliana ntafanya kazi tusipokubaliana ntarudi nyumbani”, anasema kocha huyo wa zamani wa African Sports.

Baadhi ya wachezaji waliopita mikononi mwa Aluko nio Juma Jabu, Ramadhani Chombo Redondo, Hamadi Mbumba

Kama mambo yatakwenda vizuri atakuwa ni mtanzania wa pili kufundisha nchini Kenya wa kwanza akiwa ni Sunday Kayuni aliyewahi kuinoa AFC Leopord katika miaka ya 1999.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here