Home Kitaifa JONAS MKUDE KAWAPA NENO MASHABIKI WA SIMBA KUHUSU UBINGWA WA VPL 2015-16

JONAS MKUDE KAWAPA NENO MASHABIKI WA SIMBA KUHUSU UBINGWA WA VPL 2015-16

1666
0
SHARE

Jonas Mkude

Kiungo wa Simba na nahodha msaidizi Jonas Mkude amewaomba mashabiki wa timu yake kutoka tamaa mapema kuhusu mbio za ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwasababu chochote kinaweza kutokea licha ya kuwa na gap kubwa la pointi kati yao na Yanga ambao ndiyo vinara wa ligi.

“Matokeo ya draw kwenye mchezo wetu dhidi ya Azam tumeyapokea kwa mikono miwili, mchezo wa mpira ni wa kupambana tumejitahidi na wenzetu walikuwa wakicheza kwa kutafuta pointi tatu lakini tunashukuru kwa hiki tulichokipata na tutaendelea kupamabana hadi dakika ya mwisho”, anasema nyota huyo zao la timu ya Simba ya vijana.

“Kuhusu mbio za ubingwa, mashabiki hawatakiwi kukata tamaa sisi tutaendelea kupigana hadi dakika ya mwisho hakuna mtu anaejua nini kitatokea huko mbele. Mashabiki wawe pamoja na sisi katika vipindi vyote vya furaha na huzuni”.

“Sisi hatuiangalii Yanga, kama itachukua ubingwa sawa lakini sisi tunapambana kwa ajili ya Simba”, anasisitiza Mkude.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here