Home Kitaifa WAKATI SIMBA IKIBANWA NA AZAM, MWINYI KAZIMOTO ALIKUWA AKISHEREKEA NDOA

WAKATI SIMBA IKIBANWA NA AZAM, MWINYI KAZIMOTO ALIKUWA AKISHEREKEA NDOA

1162
0
SHARE

FB_IMG_1462121411124

Kiungo mkongwe wa wekundu wa Msimbazi Simba Mwinyi Kazimoto, hakuwepo kwenye kwenye kikosi cha Simba kilichocheza dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi kutokana na kuwa mapumzikoni kufuatia kufunga ndoa Jumamosi April 30.

Mwinyi amefunga ndoa jana na Bi. Regina maeneo ya Kongowe nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, hivyo alipewa mapumziko na klabu yake kwa ajili ya kukamilisha taratibu za ndoa yake.

FB_IMG_1462121439007

Kiungo huyo wa timu ya taifa amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Msimbazi kutokana na uwezo wake wa kuchezesha timu pamoja na kupiga pasi za mwisho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here