Home Dauda TV VIDEO: LEICESTER ILINYIMWA TUTA ILI ISITANGAZE UBINGWA OT?

VIDEO: LEICESTER ILINYIMWA TUTA ILI ISITANGAZE UBINGWA OT?

471
0
SHARE

Man Utd vs Leicester 1

Kwanini haikuwa penati?

Baada ya mchezo kati ya Manchester United vs Leicester City kumalizika story kubwa kwenye mindao ya kijamii ilikuwa ni tuta ambalo Leicester walinyimwa pengine ndiyo lingezaa goli la pili na kuwapa ubingwa wakali hao wa King Power.

Man Utd vs Leicester

Wakiwa nyuma kwa goli moja kwenye dimba la Old Trafford baada ya Anthony Martial kutangulia kuifungia United, inawezekana The Foxes wangeeenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 2-1.

Wes Morgan aliisawazisha Leicester katikati ya kipindi cha kwanza, huku vinara wao wa ligi wakinyimwa tuta la wazi dakika ya 40 kipindi cha kwanza.

Beki wa kushoto wa Manchester United Marcos Rojo alikuwa na wakati mgumu kipindi cha kwanza, na huenda angesababisha penati baada ya kumzibia njia Mahrez akiwa ndani ya box.

Rojo hakuupata mpira lakini alimzuia star huyo wa Algeria lakini mwamuzi Michael Olivier alipeta.

Shuhudia video hapa chini kisha dondosha comment yako kama idhani lilikuwa ni tuta au haikuwa tuta.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here