Home Ligi EPL MASHABIKI WA MAN UTD WAITUHUMU MAN CITY KUTETEA KIBARUA CHA VAN GAAL...

MASHABIKI WA MAN UTD WAITUHUMU MAN CITY KUTETEA KIBARUA CHA VAN GAAL OLD TRAFFORD

565
0
SHARE

Man city-aibu

Premier League ni ligi ya aina yake, wakati unafikiria timu iko nje ya top four wapinzani wao wanaweza kuwarejesha tena kwenye reli ya kuwania nafasi hiyo ambayo inatoa fursa kwa vilabu hivyo kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Sare ya kufungana goli 1-1 kati ya Manchester United vs Leicester City siku ya Jumapili iliendelea kuwa na matumaini kwa United kumaliza ndani ya top four na kupata nafasi ya kucheza michuano ya Champions League.

Baada ya sare hiyo kwenye uwanja wa Old Trafford, Louis van Gaal na Wayne Rooney walikiri kwamba, wanahitaji kushinda michezo yao yote iliyosalia na hata sare yao dhidi ya vinara hao wa ligi yalikuwa ni matokeo mabaya kwao.

Game ya jioni kati ya Southampton dhidi ya  Manchester City iliibua matumaini kwa Lois van Gaal na Manchester United.

City walijikuta wakiangukia pua ugenini kwa kipigo kikali kutoka kwa Southampton huku Sadio Mane akitumbukia wavuni mara tatu.

Mane amekuwa moto na baridi msimu huu, lakini mshambuliaji kuyo wa Southampton alitumia faida ya kikosi dhaifu cha Man City kutokana na wahezaji wengi wa kikosi cha kwanza kupumzishwa kwa ajili ya mechi ya nufu fainali ya pili ya Champions League dhidi ya Real Madrid siku ya Jumatano kwenye uwanja wa Bernabeu.

Manchester City wanafaida ya kubwa ya tofauti ya magoli ukilinganisha na Manchester United lakini kwa sasa wanatofautishwa na pointi nne pekee lakini wakati huo Man United ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Mchezo huo wa mkononi utakuwa dhidi ya West Ham kwenye uwanja wa Upton Park huku wagonga nyundo hao wa London pia wakipambana kumaliza wakiwa nafasi ya nne.

Manchester City wao mechi yao ngumu ni dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wao wa nyumbani Etihad Jumapili ijayo mechi ambayo si nyepesi kwa timu zote kutokana na nafasi zilizopo huku zote zikihitaji matokeo kwa ajili ya kujihakikishia kumaliza kwenye nafasi nne za juu kwenye ligi.

Inawezekana mbio za kuwania ubingwa wa Premier League zikamalizika Jumatatu usiku, lakini Jumamosi ijayo mbio za kuwania nafasi nne za juu bado zitaendelea.

Lakini cha kushangaza mashabiki wa Manchester United wanakilaumu (kikosi chao kwa kushindwa kuifunga Leicester City), Louis van Gaal (kwa matokeo mabovu ya msimu huu) na Manchester City (kwa kuirejesha timu yao kwenye mbio za nafasi ya nne) kwani Van Gaal akifanikiwa katika hilo huenda asifukuzwe ndani ya United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here