Home Entertainment AFANDE SELE: KAMA SI UPENDO WA MAHREZ KWA SAMATTA, STARS ILIBIDI IFE...

AFANDE SELE: KAMA SI UPENDO WA MAHREZ KWA SAMATTA, STARS ILIBIDI IFE 10-0

1024
0
SHARE

Afande Sele

Mkongwe wa Bongo Flavor nchini Selemani Msindi maarufu kwa jina la Afande Sele amesema soccer ni miongoni mwa michezo yenye upendo wa hali ya juu huku akitoa sababu kadhaa katika kuthibitisha hilo.

Afande Sele ameandika ujumbe kupitia account yake ya Instagram  ‘afandeseletz’ akielezea namna mchezo huo na watu wake walivyotawaliwa na upendo wa kweli kwa kuonesha matukio mawili yanayothibitisha hilo. Tukio la kwanza ni Daniel Alves kujitolea sehemu yake ya ini kumpa beki mwenzake Eric Abidal waliyecheza pamoja kwenye klabu ya FC Barcelona ambaye aligundulika kuwa na tatizo la ini na alihitaji apandikizwe kipande cha ini kutoka kwa mtu mwingine.

Tukio la pili ambalo Afande Sele anaendelea kuonesha kuwa mchezo wa soka ulivyotawaliwa na upendo ni juu ya ile mechi ya marudiano kati ya Algeria vs Tanzania ambapo Tanzania ilipigwa goli 7-0 ugenini. Afande Sele anasema kama isingekuwa Samatta kuhurumiwa na Riyad Mahrez (mchezaji wa timu ya taifa ya Algeria na klabu ya Leicester City ya England) basi Stars ilikuwa itandikwe zaidi ya magoli hayo.

Huu hapa ni ujumbe aliouandika Afande Sele kupitia account yake y Instagram wakati akijaribu kuonesha namna mchezo wa soka ulivyotawaliwaliwa na upendo wa kweli.

Upendo ni karama ambayo Mungu amempa mwanadamu ijapokuwa ni wanadamu wachache wenye upendo na soccer ndiyo mchezo wenye upendo mkubwa, Eric Abdal alipopata tatizo la figo Daniel Alves alijitolea kumtolea Eric Abidal figo hili ni jambo ambalo siwezi kulisahau (Alves alijitolea ini na sio figo kumpa Abidal ambaye alikuwa na tatizo hilo)

Sometimes you will never know the value of a moment until it becomes a memory. Stars ilifungwa 7 pale Algeria..MAHREZ alitoa pasi 3 za mwisho..Baada ya kutoa pasi ya mwisho kwenye lile goli la 7..wenzie wakiwa wanashangili, yeye alikuwa akimtazama Mbwana Samatta kwa jicho la huruma…Baadaye akawaambia wenzie sipigi tena pasi yoyote ya mwisho..goli 7 zinatosha.

NA HII NAIFANYA KWA AJILI YA KULINDA HESHIMA YA HUYO MCHEZAJI WA KITANZANIA ALIYEVAA JEZI NO 10…Akimaanisha Samatta. Maana MAHREZ alikuwa amezitzama sana clip za Mbwana kabla ya ile mechi yao ya marudiano…inamaana bila uwepo wa Mbwana Samatta Stars ingekufa hata 10-0 siku ile.

Afande Sele

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here