Home Kitaifa IJUE SAGRADA ESPERANCA ‘MWADUI YA ANGOLA’ AMBAYO ITACHEZA NA YANGA KOMBE LA...

IJUE SAGRADA ESPERANCA ‘MWADUI YA ANGOLA’ AMBAYO ITACHEZA NA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO

1040
0
SHARE

Esparenca

Na Athumani Adam

  • Esperanca kwa sasa wanafundishwa na kocha kutoka Serbia, Zoran Mackic.
  • Wana wachezaji watano raia wa kigeni, wareno wawili, wakongo wawili na mghana mmoja.
  • Timu hii inatoka mji wa Dundo, mji wenye utajiri wa madini ya dhahabu na almasi.

Grupo Desportivo Sagrada  Esperanca  kutoka Angola wamefikia tena rekodi yao kwenye michuano ya ngazi ya vilabu barani Afrika. Mara ya mwisho kuweka rekodi yao ya juu kwenye michuano hii ilikua mwaka 2005 pale walipotolewa na Asec Abidjan ya Ivory Coast kwa jumla ya magoli 3-2 raundi ya 16 bora klabu bingwa barani Afrika.

Mwaka huu watacheza na Yanga ya Tanzania kwenye raundi ileile ya 16 bora lakini siyo klabu bingwa Afrika bali ni kombe la shirikisho. Esperanca wamefanikiwa kukutana na Yanga baada ya kutolewa na Vita Klabu ya Jamuhuri ya  Kongo ambapo  Yanga walitupwa nje na Al Alhy ya Misri kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika.

Kuelekea mchezo wa kwanza kati yao ambao utachezwa kati ya Mei 6 hadi 8 jijini Dar es Salaam kabla ya marudiano huko Angola wiki mbili baadaye makala hii inakupa mambo muhimu kuhusu klabu hii ya Angola.

Historia Fupi Ya Esperanca

Esperanca ilianzishwa 22/12/1976 mjini Dundo, kwenye jimbo la Lunda Norte Nchini Angola. Jimbo hili ambalo Esperanca wanatoka kwa Kaskazini Mashariki limepakana na Jamuhuri ya Kongo, lina sifa ya kuwa na madini mengi ya dhahabu na almasi, hivyo Esperanca kwa Tanzania unaweza kuifananisha na Mwadui FC ya Shinyanga inayomilikiwa na mgodi wa almasi.

Segrada Esperanca ni neno la kireno lenye maana ya ‘Matumaini Takatifu’ (sacred hope), hivyo kutokana na wamiliki wa klabu hii, kampuni ya madini ya Diamond Company Diaming ambayo kwa sasa kampuni hii inaitwa Endima kulipenda shairi la aliyekuwa rais wa Angola kipindi hicho Agustino Neto, shairi ambalo lilitwa Segrada Esperance wakaamua kuipa timu yao jina la shairi hilo.

Uwanja wao wa nyumbani ni Estadio Segrada Esperanca wenye uwezo wa kubeba jumla ya watazamaji 3000.

Mafanikio ndani ya Angola

Esperanca ndani ya Angola wamefanikiwa kunyakua vikombe vitatu hadi sasa. Ligi ya Angola iitwayo Girabola  wametwaa mara moja mwaka 2005 wakati kombe la FA wamechukua mara mbili mwaka 1988 na 1999.

Mashindano ya CAF

Esperanca hawana mafanikio makubwa sana kwenye michuano ya Caf, mwaka 2005 walifika hatua ya 16 bora mashindano ya klabu bingwa Afrika, pia waliishia hatua za awali za kombe hili mwaka 2006.

Mwaka 1992, 1998 walishiriki mashindano ya kombe la shirikisho ambapo waliishia raundi ya pili, mwaka 1992 na mwaka 1998 waliishia raundi ya kwanza.

Pia Esperanca waliishia raundi ya pili mwaka 1989 na 2000 kwenye  kombe la washindi barani Afrika ambalo kwa sasa halipo tena.

Wachezaji wa nje

Kwenye kikosi cha sasa timu hii ina wachezaji wakigeni watano. Wachezaji hao ni golikipa Johhy mwenye miaka 34 kutoka Jamuhuri ya Kidemoklasia ya Kongo, mlinzi wa kulia Zibakaka kutoka Kongo umri miaka 22, pia kuna mlinzi mwingine kutoka Ghana anaitwa Seth umri miaka 26 pamoja na wachezaji wawili kutoka Ureno kiungo Oliveira miaka 32 na mshambuliaji Ary mwenye miaka 27.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here