Home Kitaifa TAMBWE AMESEMA KWANINI ‘ALINUNA’ KUMPISHA BUSUNGU MISRI

TAMBWE AMESEMA KWANINI ‘ALINUNA’ KUMPISHA BUSUNGU MISRI

1640
0
SHARE
Huu ndiyo mpira aliopewa Tambwe kwenye mchezo wa Yanga vs Majimaji baada ya kupiga hat-trick, mpira huu si miongoni mwa mipira inayochezewa kwenye ligi msimu huu

Huu ndiyo mpira aliopewa Tambwe kwenye mchezo wa Yanga vs Majimaji baada ya kupiga hat-trick, mpira huu si miongoni mwa mipira inayochezewa kwenye ligi msimu huu

Kama uliufatilia mchezo wa klabu bingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Al Ahly siku ya Jumatano April 20, basi utakuwa uliona namna mshambuliaji wa timu hiyo Amis Tambwe alivyochukizwa baada ya kufanyiwa mabadiliko ili kumpisha Malimi Busungu wakati huo matokeo yakiwa ni sare ya goli 1-1.

Baada ya Yanga kuwasili kuwasili jijini Dar, shaffihdauda.co.tz ikataka kujua ni kwanini Tambwe alionekana kuchukizwa na uamuzi wa benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Hans van Pluijm kuamua kumpumzisha na nafasi yake ichukuliwe na Busungu.

“Unajua kama siku unajisikia kucheza halafu mwalimu anakutoa lazima ujisikie hasira, kweli nilikasirika sikuile kutolewa uwanjani”, anasema Tambwe ambaye alionekana wazi kuchukizwa na mabadiliko hayo wakati akitoka nje ya uwanja.

Kwasasa mambo ya klabu bingwa yanawekwa kando kwasababu tayari Yanga ipo nje ya michuano hiyo lakini kutokana na kutolewa kwao wakiwa hatua ya 16 bora, wanadondokea kwenye kapu la kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya makundi kwenye kombe la shirikisho.

Yanga imepangwa na Sagrada Esparanca ya Angola, Tambe anasema maandalizi mazuri na kujituma kutawafanya wafuzu kucheza hatua ya makundi ambayo ndiyo malengo yao kwa sasa.

“Ni kujituma unajua siku zote timu zikifika hatua ya 16 bora huwa mara nyingi zinakuwa ngumu, kwahiyo tuntakiwa kupata muda kujiandaa vizuri ili tufuzu kwenye hatua ya makundi na hayo ndiyo malengo yetu kama timu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here