Home Kimataifa TOTTI ADHIHIRISHA NG’OMBE HAZEEKI MAINI

TOTTI ADHIHIRISHA NG’OMBE HAZEEKI MAINI

622
0
SHARE

Totti

Story kubwa kwenye ligi ya Serie A ni mfalme wa AS Roma Francesco Totti kufunga goli la ushindi kwa timu yake alipotokea benchi kuchukua nafasi ya Keita.

Babu huyo wa miaka 39 jana usiku aliingia uwanjani akitokea benchi na kuubadili mchezo, wakati Totti anaingia dakika ya 85 Torino ilikuwa ikiongoza kwa magoli 2-1 mbele ya Roma.

Legend huyo wa Roma aliifungia timu yake bao la kusawazisha akiunganisha mpira wa adhabu ndogo na kuufanya mchezo kuwa sare ya magoli 2-2.

Mkongwe huyo aliihakikishia ushindi timu yake dakika ya 89 na mchezo huo kumalizika kwa Roma kushinda kwa magoli 3-2.

Akiwa hapati nafasi ya kutosha kucheza kwenye kikosi cha Roma, kuna uwezekano mkubwa msimu huu ukawa ni wa mwisho kwa Totti kuichezea klabu hiyo aliyodumu nayo katika maisha yake yote ya soka.

Usiku wa jana Totti umemfanya afikishe jumla ya magoli 303 tangu ameanza kuicheza klabu Roma.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here