Home Kimataifa SUAREZ APIGA BAO 4 MSN IKIREJEA ONLINE

SUAREZ APIGA BAO 4 MSN IKIREJEA ONLINE

530
0
SHARE

Suarez

Baada ya kupita kwenye kipindi cha ukame wa kutopachika magoli siku za hivi karibuni wakati form ya Barcelona ilipoyumba, Luis Suarez mara yake ya mwisho kufunga ilikuwa ni kwenye mechi ya kwanza ya robo fainali ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid.

Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay amerejea kwenye reli kwa kasi ya ajabu baada ya kuzama wavuni mara nne wakati Barca ikiisambaratisha Deportivo La Coruna kwa bao 8-0 katika mchezo wa La Liga uliochezwa Jumatano usiku.

Wakati huo Suarez akiwa amehusika kwenye magoli 7 ya Barcelona kwa kupiga assist 3 na kukwea hadi kileleni mwa chart ya wachezaji waliotoa assist nyingi.

Story kubwa ni Suarez kutupia bao nne ambazo zimemfanya kuongeza presha kwa Cristiano Ronaldo mwenye magoli 31 kwenye mbio za kuwania tuzo ya ufungaji bora ya La Liga (Pichichi)

Magoli hayo yanamfanya Suarez kufikisha jumla ya magoli 30 ndani ya La Liga huku akiwa amefunga magoli 49 katika michuano yote katika mechi 49 za mashindano yote aliyocheza msimu huu.

Leo Messi, Neymar, Rakitic pamoja na Marc Bartra kila mmoja alizama kambani mara moja kuifungia Barcelona kutokana na ubovu wa safu ya ulinzi ya Deportivo.

Ushindi wa Atletico Madrid na Real Madrid unamaanisha mbio za ubingwa wa La Liga bado ziko wazi kwa timu hizo tatu za juu. Barca imeungana na Atletico kufikisha pointi 79 pointi moja mbele ya Real iliyo nafasi ya tatu kwa pointi zake 78 huku vilabu vyote vikiwa visaliwa na michezo minne.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here