Home Kimataifa RONALDO AKIMBIA UWANJA MADRID IKIICHAPA VILLAREAL 3-0

RONALDO AKIMBIA UWANJA MADRID IKIICHAPA VILLAREAL 3-0

543
0
SHARE
PARTIDO ENTRE EL REAL MADRID Y EL VILLARREAL CELEBRADO EN EL ESTADIO SANTIAGO BERNABEU

PARTIDO ENTRE EL REAL MADRID Y EL VILLARREAL CELEBRADO EN EL ESTADIO SANTIAGO BERNABEU

Real Madrid imeshinda mchezo wake wa Jumatano usiku dhidi ya Villareal kwenye uwanja wake wa Bernabeu na kuweka hai matumaini yao kwenye mbio za taji la La Liga.

Mashaiki wa Madrid walimshuhudia star wa timu yao Cristiano Ronaldo akitoka nje ya uwanja kutokana na maumivu ya nyama za paja kabla ya mechi kumalizika.

Chakushangaza ni kwamba, Ronaldo aliondoka uwanjani wakati mchezo unaendelea bila kumwambia mtu yeyote, Ronaldo alipitiliza moja kwa moja hadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo zikiwa zimesalia dakika chache mchezo kumalizika.

Wapenzi wa Madrid bado wanamatumaini wakiamini nyota wao hana tatizo kubwa, na ilikuwa ni presha katika kuwania tuzo ya Pichichi kwa nyota huyo ambaye hakufunga goli kwenye mchezo huo huku mpinzani wake Suarez akimsogelea kwa tofauti ya bao moja baada ya kutupia bao nne na kufikisha magoli 30 goli moja nyuma ya Ronaldo.

Mashabiki wa Manchester City kwa upande mwingine watakuwa wakimwombea mabaya Ronaldo ili timu yao itakapokutana na Madrid kwenye nusu fainali ya Champions League wiki ijayo asiwepo uwanjani.

Ronaldo aliisaidia Madrid kufuzu hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kupiga hat-trick kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Wolfsburg, madaktari wa Madrid watakuwa wanafanya kila njia kuhakikisha star wao anarejea uwanjani mapema iwezekanavyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here