Home Kimataifa WAARABU WAENDELEA KULITESA SOKA LA TANZANIA

WAARABU WAENDELEA KULITESA SOKA LA TANZANIA

601
0
SHARE
Mchezaji wa Yanga Issoufou Boubacar akiwa chini huku wachezaji wa Al Ahly wakiondosha mpira kwenye eneo lao la hatari

Mchezaji wa Yanga Issoufou Boubacar akiwa chini huku wachezaji wa Al Ahly wakiondosha mpira kwenye eneo lao la hatari

Baada ya Azam FC kufungashiwa virago na waarabu wa Tunisia timu ya Esperance kwa kipigo cha magoli 3-0, April 20 ilikuwa zamu ya Yanga ambao walikuwa ni wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya Afrika.

Yanga imetupwa nje ya michuno ya vilabu bingwa Afrika kufuatia kufungwa ugenini kwa magoli 2-1 na timu ya Al Ahly kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, Misri.

Al Ahly walianza kuopata bao la kuongoza dakika ya 53 kipindi cha pili kabla ya Donald Ngoma kuirejesha Yanga mchezoni kwa kufunga bao kwa kicha dakika ya 67 akiunganisha vema pasi ya Juma Abdul.

Al Ahly ilijihakikishia ushindi na kufuzu kwa hatua ya makundi kufuatia kupachika bao la pili lililoizamisha Yanga dakika ya mwisho ya nyongeza 90+5 lililoitupa Yanga nje ya mashindano ya vilabu bingwa Afrika.

Kwa mujibu wa kanuni za CAF, timu zilizotolewa kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya mabingwa Afrika, zinakutana na timu washindi wa wa hatua ya 16 bora kutoka kombe la sirikisho. Kwa maana hiyo, Yanga inaangukia katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here