Home Kimataifa LIUZIO: ZESCO UNITED HUTOA DOLA 1000 KAMA POSHO YA WACHEZAJI KWA GAME...

LIUZIO: ZESCO UNITED HUTOA DOLA 1000 KAMA POSHO YA WACHEZAJI KWA GAME YA CAF

648
0
SHARE
Juma Liuzio-Mshambuliaji wa ZESCO United ya Zambia
Juma  Liuzio-Mshambuliaji wa ZESCO United ya Zambia
Juma Liuzio-Mshambuliaji wa ZESCO United ya Zambia

Na Baraka Mbolembole

Ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Stade de Mallien Bamako jana Jumanne umeipeleka timu ya Zesco United ya Zambia katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika. Mabingwa hao wa Zambia waliishia hatua ya pili mwaka mmoja uliopita lakini safari hii wametinga kwa kishindo hatua ya 8 bora.

Hiyo ni fursa nyingine muhimu kwa kijana wa Kitanzania, mshambulizi Juma Ndanda Liuzio kutangaza kipaji chake katika michuano hiyo mikubwa na yenye utajiri zaidi upande wa vilabu barani Afrika. Zesco imefuzu kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-2 (walishinda 3-1 game ya kwanza ugenini nchini Mali.)

Nimefanya mahojiano na mshambulizi huyo ( Luizio) leo Jumatano. Unataka kujua ni kwani Zesco imefuzu kwa hatua ya makundi? Shuka nami hapa…www.shaffihdauda.co.tz inakuletea kwa ukaribu habari za wachezaji wetu wa kitanzania wanaocheza ng’ambo kwa sasa ..

www.shaffihdauda.co.tz: Hongereni kufuzu 8 bora, ni mara ya ngapi kwa timu yenu?

Juma Ndanda Liuzio: Tangu ( 2014)  mimi nifike hapa  hii ni mara ya kwanza.

www.shaffihdauda.co.tz: Hali ikoje hivi sasa hapo Zambia baada ya timu yao kufuzu kwa 8 bora?

Juma Ndanda Liuzio: Huku kupo poa sana watu wamehamasika sana na wanafuraha sana

www.shaffihdauda.co.tz: Nini siri ya mafanikio ya klabu yako na unachukuliaje kucheza michuano hiyo?

Juma Ndanda Liuzio: Ni ushirikiano na umoja wetu wachzaj viongozi na kujituma sana na malengo yetu pia. Nimefurahi ni mashindano makubwa barani Afrika na kitu ambacho kilikuwa kwenye ndoto zangu siku moja, nimefurahi sana.

www.shaffihdauda.co.tz: Umejifunza nini kuhusu klabu za nje zinavyojiandaa katika game za CAF?

Juma Ndanda Liuzio: Nimejifunza wenzetu wapo serious sana katika club bingwa hasa viongozi wanajaribu ‘kuwa-push’ wachezaji katika  kila kitu.

www.shaffihdauda.co.tz: Kuwasukuma kwa namna gani labda?

Juma Ndanda Liuzio: Wanatoa posho kubwa kwanza

www.shaffihdauda.co.tz: Kwa game ya CAF posho inakaribia kiasi gani na unadhani hiyo ni sababu pekee ya Zesco kufanya vizuri msimu huu?

Juma Ndanda Liuzio: Posho dola 1000 inachangia ila pia wachezaji wote wana malengo ya kufika mbali, So tunahamasa pia sisi wenyewe ukiondoa posho.

www.shaffihdauda.co.tz: Baada ya kutolewa msimu uliopita, je, timu ilisajiliwa upya au? namaanisha kama wachezaji zaidi wapya walisajiliwa.

Juma Ndanda Liuzio: Yap,  imesajili wachezaji wanne tu maana kuna wachezaji ambao waliondoka pia.

www.shaffihdauda.co.tz: Kitu gani watanzania tutarajie kutoka kwako?

Juma Ndanda Liuzio: Kikubwa nitajitahidi kipindi hiki nilichopona nipambane ili niisaidie timu kufika mbali zaidi ya  hapa.

www.shaffihdauda.co.tz: Juma sisi tumefurahishwa na maendeleo ya timu yako na tuna imani utafanya vizuri huko uliopo

Juma Ndanda Liuzio: Inshaallah kaka dua zenu muhmu naamini tutafika tu tunapotaka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here