Home Ligi BUNDESLIGA Vita ya ufungaji magoli: MSN, BBC, waendelea kuumana kwa tofauti ya goli...

Vita ya ufungaji magoli: MSN, BBC, waendelea kuumana kwa tofauti ya goli moja

1205
0
SHARE

Safu za ushambuliaji za ligi kubwa barani ulaya zinaendelea kuchuana vikali kuelekea mwishoni mwa msimu huu wa 2015/16.

 La Liga safu za ushambuliaji za Real Madrid na FC Barcelona mchuano unaendelea kushika hatamu, wakati BBC – Benzema, Bale na Cristiano Ronaldo wakiwa wamefunga magoli 69 kwenye ligi pekee yake, MSN – Messi, Suarez na Neymar wamefunga magoli 70.

Ronaldo anaongoza kwa kufunga katika chati ya wafungaji bora akiwa na magoli 31 katika mechi 33 akiwa anaitafuta Pichichi yake ya 4 mfululizo, Benzema akiwa na magoli 22 katika mechi 23, Bale amefanikiwa kufunga magoli 16.

BBC wote walifunga katika mchezo dhidi ya Getafe jumamosi hii, wakati goli la Messi la jumapili vs Valencia likawafanya MSN kutimiza magoli 70 kwenye La Liga msimu. Messi akifunga magoli 23 katika mechi 28, Suarez akifunga magoli 36 katika mechi 30 huku Neymar akiwa na magoli 21.

 Safu ya ushambuliaji ya Benfica ya washambuliaji wawili Jonas na Kostas Mitroglou wamefunga magoli 48.


Kwenye Ligue 1, combination ya Zlatan Ibrahimovic na Edinson Cavan wao wamefunga magoli 47 katika ligi hiyo na timu yao ya Paris Saint Germain.


Na Bundesliga, wachezaji wa Bayern Munich Thomas Muller na Robert Lewandowski wamefunga pamoja magoli 46.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here