Home Entertainment HABARI NJEMA KWA VIJANA: AZAM TV IMEWASOGEZEA FURSA MIKONONI MWENU

HABARI NJEMA KWA VIJANA: AZAM TV IMEWASOGEZEA FURSA MIKONONI MWENU

864
0
SHARE

DSC_1006

Habari njema kwenye tasnia ya filamu Bongo ni uzinduzi wa mradi wa kusaka vipaji vya waigizaji pamoja na ma-camera person, mradi huo unakwenda kwa jina la ‘Kiwanda cha Filamu’.

Deal hilo linasimamiwa na Azam TV kupitia channel yake ya ‘Sinema Zetu’, kitu kizuri kuhusu mpango huo ambao umelenga kuwatoa wasanii chipukizi ni uwepo wa mwigizaji mkongwe na maarufu kwenye Bongo Movies Susan Lewis ‘Natasha’ pamoja na Issa Mbura ambaye amejizolea umaarufu baada ya kung’ara kwenye movie inayoiitwa ‘Home Coming’.

aZAM TV 1

Mr. Mbura na Natasha watakuwa ni majaji watakaosimamia zoezi zima la kuwapata waigizaji wenye vipaji pamoja na camera persons watakaofuzu katika shindano hilo la kutafuta waigizaji na wapiga picha za video.

Azam TV

Takribani washiriki 200 watafanyiwa usaili Jumatano April 20 maeneo ya Coco-Beach kwa ajili ya kuwapata washindi ambapo wanatakiwa waigizaji 20 na camera persons wawili.

Azam TV 2

Washindi watapata fursa ya kushiriki katika tamthilia itakayowashirikisha ma-star wengine kutoka Bongo tamthilia ambayo inataji kuanza kurushwa mwezi July mwaka huu.

Azam TV3

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here