Home Kitaifa MSUVA: UKIKUBALI KUSHANGILIWA, KUBALI KUZOMEWA

MSUVA: UKIKUBALI KUSHANGILIWA, KUBALI KUZOMEWA

637
0
SHARE
Msuva akitoa neno kwa watu waliohudhuria birthday part yake usiku wa December 3, 2015

Msuva akitoa neno kwa watu waliohudhuria birthday part yake usiku wa December 3, 2015

Mara baada ya game ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar, nimekutana na winga wa Yanga Simon Msuva na kupiga nae story kuhusu game yao na Mtibwa ambapo yeye alifunga bao pekee lililoirejesha timu yake kileleni mwa ligi baada ya kuenguliwa na mahasimu wao Simba SC.

Nimemuuliza Msuva anajisikiaje kuhusu mashabiki wa timu yake kumzomea mara kadhaa wanapohisi amekosea kitu uwanjani na yeye hali hiyo inamuathiri vipi anapokuwa uwanjani? Jamaa alikuwa na majibu yafuatayo…

“Mimi kazi yangu ni uwanjani siyo mashabiki, shabiki anakuja kwasababu yangu, mimi nafanya kazi shabiki atashangilia kama kazi ni nzuri ikiwa mbaya hawezi kushangilia. Lakini unapokubali kushangiliwa pia kubali kuzomewa, mimi kuzomewa kwangu naona kawaida tu ila ninachoangalia ni kutekeleza maagizo niliyopewa na kocha”, anasema Msuva ambaye aliibuka mchezaji na mfungaji bora wa ligi msimu uliopita 2014/15.

Sikuishia hapo, nikamuuliza tena nini siri ya mafanikio ya Yanga kushinda mechi zake za hivi karibuni ikiwa ni pamoja na zile za michuano ya FA Cup wakati imeshuhudiwa majirani zao wakisukumwa nje ya mashindano na timu kutoka mkiani mwa ligi?

“Sisi wachezaji lazima tujiandae na kupambana na kufanya kitu cha ziada kabloa hata ya maelekezo ya kocha kwasababu mechi zote zilizobaki ni ngumu na ukiangalia bado kuna mechi nyingine tutaenda kucheza mikoani kwahiyo ni lazima tuhakikishe tunapata pointi. Sisi wachezaji tunahamasishana kutokana na mechi zenyewe, tuongeze mazoezi binafsi ili tukifika uwanjani tuwe fit zaidi nadhani pia kinatusaidia”, anasema dancer huyo wa zamani kutoka nyumba ya kulea na kukuza vipaji vya muziki THT.

Mwisho sikuacha kumuuliza kuhusu mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Ahly ambao Yanga watacheza wakiwa ugenini huku wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya kufungana 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Bongo, yeye amejipangaje kuhakikisha Yanga inasonga mbele?

“Kuhusu huo mchezo naomba watanznia watuombee, mchezo ni mgumu siwezi kuuzungumzia ila tutapambana kwasababu ile timu si ya kubeza”, alimaliza mhezaji huyo ambaye alianzia benchi kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Al Ahly uliochezwa uwanja wa taifa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here